Na Bashir Nkoromo
IKIWA sasa ni takriban miaka miwili tangu aliyekuwa Mkurugenzi wa Tanzania One Theatre (TOT), Kampteni John Komba, kufariki Dunia, Mtoto wake Gerald John Komba, ameibuka na kutoa wimbo wa kuiunga mkono Serikali katika mapambano yake mapya dhidi ya dawa za kulenya nchini Tanzania.
Gerald aliyezaliwa mwaka 1986 jijini Dar es salaam, amesema, ameamua kutoa wimbo huo wenye maudhi ya kwaya, ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya kifo cha Baba yake, Marehemu John Komba aliyefariki Dunia, Februari 28, 2015 katika Hospitali ya TMJ, Mikocheni jijini Dar e Salaam, alikopelekwa baada ya kuzidiwa ghafla akiwa nyumbani kwake, Tangibovu kwa Komba.
Mtoto huyo wa Jihn Komba aliyekuwa mwanamuziki nguri wa utunzi na uimbaji wa nyimbo za kwaya, amesema, wimbo aliotoa nimarejeo ya wimbo ambao ulitungwa na nguri huyo, kukemea usambazaji na matumizi ya dawa za kulevya miaka zaidi ya kumi iliyopita, lakini baada ya kuurekodi haukuwahi kuimbwa na TOT wala kuchezwa kwenye vituo vya Radio au Televisheni.
Gerald ambaye amesomea Sheria katika Chuo Kikuu cha Saint Augustine kilichopo Mwanza, Tanzania, baada ya masomo ya shule ya Msingi katika shule ya Kawe "A" na shule yasekondari Mbezi Beach High school, anasema katika kuutoa wimbo huo, hakubabaisha kwa kuwa na yeye anacho kipaji cha kuimba japo amekuwa hakitumii sana. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.



Watoto wanaokwenda nchini Israel kwa matibabu ya matatizo mbalimbali ya moyo kwa msaada wa taasisi ya Save the Children Heart wakiwa na Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto Dk. Godwin Godfrey pamoja na wauguzi na wazazi wao.











