Watoto wanaokwenda nchini Israel kwa matibabu ya matatizo mbalimbali ya moyo kwa msaada wa taasisi ya Save the Children Heart wakiwa na Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto Dk. Godwin Godfrey pamoja na wauguzi na wazazi wao.
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo inasafirisha watoto nane kwenda nchini Israel kwaajili ya matibabu, watoto hao ni wenye matatizo mbalimbali ya moyo ambapo imeelezwa kwamba kati ya watoto milioni 1. 5 wanaozaliwa kwa mwaka, asilimia 0. 9 wanazaliwa na matatizo ya moyo jambo ambalo taasisi hiyo haiwezi kumudu kuwatibu wagonjwa wote.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment