Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyabiashara ndogondogo
wa eneo la Namanga wilayani Longido wakati alipotembelea Kituo cha
Pamoja cha Forodha cha Namanga Septemba 21, 2017. Kulia wake ni Mkuu wa
Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa Kituo cha
Pamoja cha Forodha cha Namanga wilayani Longido wakati alipowasili
kituoni hapo, Septemba 21, 2017 kukagua shughuli za kituo hicho Septemba
21, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Kituo cha
Pamoja cha Forodha cha Namanga wilayani Longido kituoni hapo, Septemba
21, 2017 wakati alipokagua shughuli za kituo hicho Septemba 21, 2017.
**********************
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewataka watumishi katika mipaka mbalimbali
nchini ukiwemo wa Namanga mkoani Arusha kuhakikisha wanachunguza kwa
umakini mizigo yote inayoingia ili kudhibiti uingizwaji wa silaha na
dawa za kulevya nchini.
Ametoa
agizo hilo leo (Alhamisi, Septemba 21, 2017) alipotembelea kituo cha
Pamoja cha Forodha cha Namanga wilayani Longido kilichopo kwenye mpaka
wa Tanzania na Kenya na kisha kuzungumza na wafanyabiashara ndogo ndogo.
Waziri
Mkuu amesema ni vema watumishi wa vituo vya forodha katika maeneo ya
mipaka wakawa makini kwa kuhakikisha wanadhibiti uingizwaji wa silaha
pamoja na dawa za kulevya nchini kwa sababu ndiyo zinazotumika katika
matukio ya kihalifu.
Pia
Waziri Mkuu ameziagiza mamlaka mbalimbali zinazosimamia ubora wa bidhaa
kwenye vituo vote vya Forodha nchini kuhakikisha wanachunguza bidhaa
zote na kujiridhisha ubora wake kabla ya kuruhusu kuingizwa nchini na
kutumika.
“Tusingependa
nchi yetu kuwa eneo au shimbo la kutupia bidhaa zisizokuwa na ubora
Wizara zote zinazohusika na udhibiti wa ubora wa bidhaa zihakikishe
suala la ukaguzi wa viwango vya ubora wa bidhaa zote zinazoingia nchini
linapewa kipaumbele.”
Katika hatua nyingine, Waziri
Mkuu amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Longido, Bw. Daniel Chongolo pamoja
na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Bw. Juma Mhina kukutana na
wananchi wanaofanya biashara ndogo ndogo katika eneo hilo pamoja na
viongozi wa TRA na kuwatafutia eneo lingine kwa ajili ya kufanyia
biashara zao.
Amesema
kwa kuwa wananchi hao awali walikuwa wanafanya biashara zao ndani ya
eneo hilo kabla ya kujengwa kituo hicho cha Pamoja cha Forodha, ambapo
kwasasa hawaruhusiwi kutokana na makubaliano yaliyofikiwa kati ya
Tanzania na Kenya kuhusu uendeshaji wa kituo hicho hivyo ni vema
wakawatafutia eneo jingine nje ya uzio wa kituo hicho.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment