Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia baada ya kuweka jiwe la msingi
la Mradi wa maji wa Longido mkoani Arusha Septemba 21, 2017. Wapili
kushoto ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge na
kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. Kulia ni Mbunge wa
Hanang Dkt. Mary Nagu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kuwasili
kwenye eneo la uwekaji jiwe la Msingi la Mradi wa Maji wa Longido mkoani
Arusha, Septemba 21, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho
Gambo.
Baadhi ya Wananchi wa Longido wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Mjaliwa
wakati alipozungumza kabla ya kuweka jiwe la Msingi la Mradi wa maji wa
Longido Mkoani Arusha, Septemba 21, 2017.
*****************
CHANGAMOTO
ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama wilayani Longido mkoani Arusha
kuwa historia baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuweka jiwe la msingi la
ujenzi wa mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya sh. bilioni 15.8.
Waziri
Mkuu ameweka jiwe hilo la msingi leo (Alhamisi, Septemba 21, 2017) kwa ajili ya
ujenzi wa mradi wa maji wa Longido Mjini
pamoja na kijiji cha Oltepesi ambao
chanzo chake ni kutoka mto Simba wilaya ya Hai mkoani Kilimanajro.
Amesema
Serikali kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo,
itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini watapata huduma ya maji safi na
salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.
Pia
Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge
kupeleta wataalamu wilayani Longido ambao watashirikiana na Halmashuri za
wilaya ya Longido na tarafa ya
Loliondo kutafuta vyanzo vingine
vya maji ili wananchi waweze kupata maji
ya kutosha.
Waziri
Mkuu amesema asilimia kubwa ya wananchi wa wilaya za Longido na Ngorongoro ni
wafungaji hivyo wanahitaji maji mengi watakayoyatumia katika matumizi yao ya
kawaida ya nyumbani pamoja na kunyweshea migugo.
Pia
Waziri Mkuu amewaagiza wakandarasi wote wanaotekeleza mradi huo pamoja na
miradi mingine midogo tisa katika wilaya ya Longido kutumia vifaa
vinavyotengenezwa na viwanda vya ndani ili kuunga mkono jitihada za Serikali ya
Awamu ya Tano kukuza uchumi kupitia viwanda.
Katika
hatua nyingine Waziri Mkuu amesema wananchi wanatakiwa wazingatie sheria ya
Mazingira inayozuia kufanya shughuli za kibinadamu pamoja na kujenga kwenye
maeneo yote ya vyanzo vya maji ndani ya mita 60 ili kuliepusha Taifa kugeuka
jangwa.
Kufuatia
hali hiyo Waziri Mkuu aliwaagiza watendaji wawachukulie hatua watu wote
watakaokutwa wakiendesha shughuli mbalimbali kama za kilimo, ujenzi wa makazi
na uchungaji wa mifugo ndani ya vyanzo vya maji kwa kuwa zinasababisha ukame.
Awali
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Lwenge aliwaagiza Wakandarasi
wanaojenga mradi huo kuhakikisha wanajenga kwa kuzingatia viwango vya ubora
vinavyohitajika pamoja na kumaliza kwa wakati. Mradi huo unatarajiwa kukamilika
Julai, 2018.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment