RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Wallace Karia amewateua
Makamu wa Rais wa zamani wa TFF, Athuman Nyamlani na Ahmed Mgoyi kuwa
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF.
Rais
Karia ameteua kwa kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo katika Katiba ya TFF
ikiwa ni wiki moja baada ya kupatikana kwa viongozi wa shirikisho katika
uchaguzi mkuu uliofanyika Agosti 12, mwaka huu.
Rais
Karia aliwatambulisha viongozi hao kwenye Kikao cha Kamati ya Utendaji
iliyofanyika Jumanne Agosti 22, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Katika
kikao hicho pia Rais Karia alitumia fursa hiyo kutangaza viongozi wa
kamati mbalimbali za TFF zikiwamo za kinidhamu na kisheria. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Kamati ya Nidhamu: Mwenyekiti Tarimba Abbas, Makamu Mwenyekiti, Peter Hella wakati wajumbe ni Boniface Lyamwike, Dk. Bill Haonga na Kassim Dau.
Kamati
ya Rufani za Nidhamu: Mwenyekiti ni Wakili Rahim Zuber Shaban; Makamu
Mwenyekiti, Stella Mwakingwe wakati Wajumbe ni Abbas Mtemvu, Amani
Mulika na Siza Chenja.
Kamati
ya Maadili: Mwenyekiti ni Wakili Hamidu Mbwezeleni, Makamu Mwenyekiti
ni Wakili Steven Zangira wakati Wajumbe ni Glorious Luoga, Walter Lungu
na Amin Bakhressa.
Kamati
ya Rufaa ya Maadili: Mwenyekiti ni Wakili Ebenezer Mshana; Makamu
Mwenyekiti ni DCP. Mohammed Mpinga na wajumbe ni Wakili Benjamin
Karume, George Mayawa na ASP. Benedict Nyagabona.
Kamati
ya Uchaguzi: Mwenyekiti ni Revocatus Kuuli; Makamu Mwenyekiti ni Wakili
Mohammed Mchengerwa; Wakili Edwin Mgendera; Wakili Kiomoni Kibamba na
Wakili Thadeus Karua.
Kamati
ya Rufani ya Uchaguzi: Mwenyekiti ni Kenneth Mwenda; Makamu Mwenyekiti
ni Jabir Shekimweri na Wajumbe ni Wakili Rashid Sadalla, Irene Kadushi
na Mohammed Gombati.
Kamati
ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji: Mwenyekiti ni Elias Mwanjala;
Makamu Mwenyekiti ni Wakili Malangwe Mchungahela wakati Wajumbe ni
Zakaria Hanspope, Robert Selasela, Goodluck Moshi, Mhandisi Issa Batenga
na Hamis Semka.
Kamati
ya Fedha na Mipango: Mwenyekiti ni Michael Wambura; Makamu Mwenyekiti
ni Francis Ndulane na Wajumbe ni Almas Kasongo, Pascal Kihanga,
Maximillian Tabonwa, Paul Bilabaye na Farid Abeid.
Kamati
ya Mashindano: Mwenyekiti ni Ahmed Mgoyi; Makamu Mwenyekiti ni James
Mhagama wakati Wajumbe ni Kenneth Pesambili, Shafii Dauda, Fortunatus
Kalewa na Mhandisi Andrew Makota.
Kamati
ya Ufundi: Mwenyekiti ni Vedastus Lufano; Makamu Mwenyekiti ni Issa
Bukuku na wajumbe ni Sarah Chao, Ally Mayay, Michael Bundala, Omar
Abdulkadir na Israel Mujuni.
Kamati
ya Soka la Vijana: Mwenyekiti ni Khalid Abdallah; Makamu Mwenyekiti ni
Lameck Nyambaya na Wajumbe ni Mohammed Aden, Ramadhani Nassib, Salim
Kibwana na Vicent Majili.
Kamati
ya Mpira wa Wanawake: Mwenyekiti ni Amina Karuma; Makamu Mwenyekiti ni
Rose Kissiwa na Katibu wa Kamati hiyo ni Somoe Ng’itu wakati Wajumbe ni
Zena Chande, Beatrice Mgaya, Sofia Tigalyoma, Zuhura Kapama na Nia
Mjengwa.
Kamati
ya Waamuzi: Mwenyekiti ni Saloum Chama; Makamu Mwenyekiti Joseph
Mapunda wakati Wajumbe ni Nassib Mabrouk, Leslie Liunda na Soud Abdi.
Kamati
ya Habari na Masoko: Mwenyekiti ni Dunstan Mkundi; Makamu Mwenyekiti ni
Mbasha Matutu wakati Wajumbe ni Imani Kajura, Mgaya Kingoba, Godfrey
Dilunga na Samson Mbamba.
Kamati
ya Ukaguzi wa Fedha: Mwenyekiti ni Yahya Hamad; Makamu Mwenyekiti ni
Athuman Nyamlani na Wajumbe ni Khalifa Mgonja, Japhary Kachenje, Jackson
Songoro na Benesta Rugora.
Kamati
ya Tiba: Mwenyekiti ni Dkt. Paulo Marealle; Makamu Mwenyekiti ni Dkt.
Fred Limbanga Wakati wajumbe ni Dkt. Norman Sabun, Dkt. Lisobina
Kisongo, Dkt. Eliezer Ndalama, Dkt. Elson Maeja na Violet Lupondo.
Kamati
ya Futsal na Beach Soccer: Mwenyekiti ni Ahmed Mgoyi; Makamu Mwenyekiti
ni Hussein Mwamba na Wajumbe ni Blassy Kiondo, Isaac Munisi, Didas
Zimbihile na Aaron Nyanda.
Kamati
ya Ajira: Mwenyekiti ni Issa Bukuku; Makamu Mwenyekiti ni Saloum Chama
wakati Wajumbe ni Athuman Kihamia, Mtemi Ramadhani, Noel Kazimoto na
Hawa Mniga.
Kamati ya Leseni za Klabu: Mwenyekiti ni Wakili Lloyd
Nchunga; Makamu Mwenyekiti Wakili Emmanuel Matondo wakati Wajumbe ni
Profesa Mshindo Msolla, Hamisi Kissiwa na David Kivembele.
Kamati
ya Rufaa za Leseni: Mwenyekiti Wakili Dk. Damas Ndumbaro; Makamu
Mwenyekiti ni Wakili Alex Mngongolwa Wajumbe ni Meneja wa zamani wa
Uwanja wa Taifa, Charles Matoke, Tumainiel Mlango na Ahmed Menye.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment