Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akitembelea Bonde la Ihefu Wilayani Mbarali mkoani Mbeya leo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akitembelea Bonde la Ihefu Wilayani Mbarali mkoani Mbeya leo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza na wananchi wa Ihefu.
MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala leo ametembelea Bondebla Ihefu lililopo Wilayani Mbarali mkoani Mbeya.Bondenla Ihefu ni mojanya eneo Oevu na ndipo kilipo chamzo cha maji cha mto Ruaha Mkuu
Makala katika ziara hiyo aupongeza uongozi wa Wilaya na wananchi kwa kuitikia maelekezo ya serikali ya mkoa kuhusu kulinda eneo hilo na amefurahishwa kukuta eneo hilo lipo salama hakuna mifugo,uoto wa asili umeanza kurejea na Maji kutiririka vizuri mto Ruaha.
Aidha amewaonya wananchi wachache wanaopeleka mifugo nyakati za usiku na kuzitoa alfajiri na ametangaza ulinzi na doria ya askari wa wanyama pori kufanyika saa 24.
Makalla amewataka wananchi kutofanya shughuli eneo la Ihefu kwani eneo hilo ndiyo chanzo cha mto Ruaha kwa ajili ya kutiririsha Maji kupeleka Hifadhi ya Ruaha na bwawa la Mtera.
Amesema ili kutekeleza Agizo la Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan la kurejesha Ekolojia ya mto Ruaha, huku akitaka serikali ya Mkoa itasimamia sheria ya kulinda vyanzo vya Maji , kuondoa mifugo maeneo oevu na hifadhi, kuweka alama mifugo ili kuzuia uingiaji mifugo kiholela katika Mkoa wa Mbeya.Amewatoa hofu wananchi kutosikiliza propaganda za kuhamishwa badala yake waendelee na shughuli zao za kujipatia kipato na maendeleo
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment