Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Moira wa Miguu Tanzania, Sarah Chao akila kiapo mbele ya Msajili wa Vyama vya Michezo nchini,Ibrahim Sapi Mkwawa huku akishuhudiwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mohamed Kiganja./Picha:Mroki Mroki.
Sarah aligombea nafasi ya Ujumbe huku akiwa mwanamke pekee aliyejitosa kuwania nafasi hiyo upande wa wanawake na kufanikiwa kuwapiga mweleka wapinzani wake wawili ambao ni wanaume kwenye Kanda namba 4 yenye mikoa ya Arusha na Manyara na kushinda kwa kupata kura 57 dhidi ya Omar Walii na Peter Temu waliopata kura 32 kila mmoja.
Baada ya kuapishwa, Chao alisema
kuwa anajisikia faraja kuwa mshindi na kwamba ataenda kufanya kazi kwaajili ya
maendeleo ya Arusha na Manyara lakini kwa taifa pia.
Alisema, “Ni faraja na ni ushindi wa
heshima kwangu. Nitapambana na nitafanya kazi kwaajili ya maendeleo ya soka
letu."
Wajumbe mbalimbali wakila kiapo cha maadili mbele ya Msajili
wa Vyama vya Michezo nchini,Ibrahim Sapi Mkwawa huku akishuhudiwa na
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mohamed Kiganja.
****************
Kwa upande wa Wajumbe walioshinda ni
kama ifuatayo; Kanda namba 1 ya Mikoa ya Kagera na Geita: Saloum Chama,
Kanda namba 2 inayounganisha mikoa ya Mara na Mwanza ni Vedastus
Lufano, Kanda namba 3 (Mikoa ya Shinyanga na Simiyu) ni Mbasha Matutu.
Kanda namba 4 (Mikoa ya Arusha na Manyara) mshindi alikuwa Sarah Chao
wakati Katika Kanda namba 5 inayounganisha mikoa ya Kigoma na Tabora
aliyeshinda ni Issa Bukuku.
Pia Kenneth Pesambili
alishinda kwa upande wa Kanda namba 6 yenye mikoa ya Katavi na Rukwa
wakati kwenye Kanda namba 7 inayounganisha mikoa ya Mbeya na Iringa mshindi
alikuwa ni Elias Mwanjali.
Kanda namba 8 yenye mikoa ya Njombe
na Ruvuma aliyeibuka mshindi alikuwa ni James Mhagama, Kanda namba 9 Lindi na
Mtwara alishinda Dunstan Mkundi wakati Kanda namba 10 yenye mikoa ya Dodoma na
Singida aliyeshinda ni Mohamed Aden.
Kanda namba 11, mikoa ya Pwani na
Morogoro mshindi alikuwa Francis Ndulane wakati Kanda namba 12 Kilimanjaro na
Tanga mshindi alikuwa Khalid Mohamed. Kanda iliyokuwa na ushindani mkubwa zaidi
ya ni Kanda namba 13 yenye mkoa Dar es Salaam ambapo aliyeibuka mshindi kwa
kuwabwaga wapinzani wake 11 ni Lameck Nyambaya.
RAIS WA TFF : Wallace Karia
MAKAMU WA RAIS : Michael Wambura
WAJUMBE KAMATI YA UTENDAJI
Zone 1: Saloum Chama
Zone 2: Vedastus Lufano
Zone 3: Mbasha Matutu
Zone 4: Sarah Chao
Zone 5: Issa Bukuku
Zone 6: Kenneth Pesambili
Zone 7: Elias Mwanjala
Zone 8: James Mhagama
Zone 9: Dunstan Mkundi
Zone 10: Mohamed Aden
Zone 11: Francis Ndulane
Zone 12: Khalid Abdallah
Zone 13: Lameck Nyambaya
WAJUMBE KAMATI YA UTENDAJI
Zone 1: Saloum Chama
Zone 2: Vedastus Lufano
Zone 3: Mbasha Matutu
Zone 4: Sarah Chao
Zone 5: Issa Bukuku
Zone 6: Kenneth Pesambili
Zone 7: Elias Mwanjala
Zone 8: James Mhagama
Zone 9: Dunstan Mkundi
Zone 10: Mohamed Aden
Zone 11: Francis Ndulane
Zone 12: Khalid Abdallah
Zone 13: Lameck Nyambaya
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment