WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harson
Mwakwyembeakizungumza baada ya viongozi wapya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupatikana katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Mjini Dodoma Agosti 12,2018.
Viongozi wapya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Rais TFF, Wallace Karia (kulia) akiwa na Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo, Michael Wambura wakimsikiliza Waziri mwenye dhamana ya Michezo, Dk Harrison Mwakyembe, baada ya kutangazwa washindi wa Uchaguzi wa TFF uliofanyika mjini Dodoma Agosti 12,2017.
*****************
WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Harson
Mwakwyembe aliwapongeza wajumbe kwa kufanya uchaguzi wa kistaarabu na hatimaye
kuwapata viongozi wapya wa kuliongoza Shirikisho hilo kwa miaka minne.
Pia Mwakyembe alitoa shukrani zake kwa wajumbe kutoka CAF na
FIFA, kwa ukaribu wao waliouonyesha tangu mwanzo wa mchakato wa uchaguzi mbaka kufiki
jana ambapo ndiyo ilikuwa mwisho.
“Kwakweli nawashukuru watu wote ikiwemo wajumbe wa CAF na
FIFA kutokana na ushirikiano wao mkubwa katika ucahguzi huu, lakini nawapongeza
sana wagombe walioshindwa na walioshinda kwasababu kwenye uchaguzi kuna mambo
mawili kupata na kukosa hivyo nilazima kukubali na kitu cha msingi naomba wale
walioshindwa kuwaunga mkono wenzao ili waweze kufanya kazi ya kujenga mpira wa
Tanzania kwa pamoja,”alisema Mwakyembe.
Waziri huyo wa michezo alisema anamatumaini makubwa na viongozi
wapya waliochaguliwa kwani kazi kubwa iliyopo mbele yao ni kuhakikisha soka la
Tanzania linasonga mbele na kuanzia mwakani anataka viongozi hao wawajibike
kutoa taarifa ya misada wanayopata kutoka FIFA kwenye magazeti.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment