UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la soka
Tanzania TFF, umekamilika kwa Wallece Karia kuibuka kidedea wa kiti cha Urais
baada ya kupata kura 95 (asilimia 74.22) ambazo hazikuweza kufikiwa na wagombea
wengine waliokuwa wakiwania nafasi hiyo.
Karia alikuwa Makamu wa Rais kwenye uongozi uliopita ambao
ulikwa unaongozwa na Jamali Malinzi, aliye enguliwa kwenye uchaguzi huo
kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa fedha za TFF, yeye na Katibu Mkuu wa TFF,
Selestine Mwesigwa.
Karia ameibuka mshindi katika nafasi ya Rais, baada ya
kuwashinda wapinzani wake Ally Mayayi na Shija Richard ambao wote walipata kura
tisa Iman Madega aliyepata kura nane, Fredrick Mwakalebela kura tatu na Emmanuel Kimbe aliyepata kura
moja.
Katika nafasi ya Makamu wa Rais aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la
soka Tanzania FAT sasa TFF, Richard Wambura alishinda nafasi hiyo kwa kupata
kura 85 ( asilimia 66.4) na kuwabwaga wapinzani wake Mulami Nghambi aliyepata
kura 25,Mtemi Ramadhani kura 14 na Robart Selasela aliyeambulia kura mbili.
Baada ya kuapishwa Rais Mpya wa TFF, Karia alitoa hutuba
fupi ambapo aliitaka Kamati yake kuchapa kazi kwa bidii ili kurudisha imani ya
Watanzania katika mchezo huo ambao unaongoza kwa kuwa na mashabiki wengi
nchini.
Karia alianza kwa kuwashukuru wajumbe kwa kuonyesha imani
kubwa kwake hata kumchagua yeye kuwa kiongozi mkuu wa TFF, na kuahidi
kuwatumikia kwa nguvu zake zote ili kufika kule ambako wamekusudia.
“Katika ilani yangu nina vitu 11, ambavyo vinaonekana
vidogo, lakini siyo hivyo kama wanavyodani nitahakikisha navisimamia kwa
umakini ili kurudisha mpira wa Tanzania kwenye levo inayotakiwa,”alisema Karia.
Kiongozi huyo alisema katika uongozi wake atajitahidi kutoa
mafunzo mbalimbali ikiwemo na kwa waandishi wa Habari ili waweze kufanya kazi
yao kwa umakini na wawee kusaidiana ili mambo yao yaweze kwenda sawa.
If you want to be a wise, so you need to read the daily news. I am trying to it. Thank you for sharing football news. Have you another red tea news?
ReplyDeleteGood! We need to know daily news. So we can read this blog and another news site, like this redtea.com.
Thanks