Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Saturday, 12 August 2017

MWAKYEMBE AFUNGUA MKUTANO MKUU WA TFF ATOA ONYO KWA WAGOMBEA UONGOZI

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe amewataka viongozi wapya wa Shirikisho la soka Tanzania TFF, kutanguliza maslahi ya mchezo huo mbele na sio maslahi yao binafsi.

Mwakyembe aliyekuwa Mgeni Rasmi kwenye Uchaguzi huo wa TFF, unaoendelea kwenye ukumbi wa St. Gasper mkoani Dodoma, alisema Wajumbe ambao ndiyo wapiga kura ndiyo wenye jukumu kubwa la kuhakikisha soka la Tanzania linaendelea.

“Viongozi bora huibuliwa na wajumbe makini wanaoongozwa na dhamira njema na uzalendo usiotetereka kwa vishawishi, alisema na kutaka mgombea atakayeibuka kuwa mshindi kula kiapo kuwa atafanya kazi yake wa uadilifu na kwa manufaa ya watanzania.BOFYA HAPA KUONA MATUKIO ZAIDI.

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
Baadhi ya wajumbe wakiwa katika mkutano huo.
Wajumbe wakifuatilia mkutano huo.
Kaimu Rais wa TFF, Wallace Karia akizungumza.
Mwakilishi wa FIFA katika mkutano huo akizungumza.
Wajumbe wakifuatilia mkutano.
Mazingira ya kazi kwa waandishi wa Habari katika mkutano huo hayakuwa rafiki. Hapa wakinasa sauti katika moja ya spika ukumbini humo.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF ambao ni Viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Wanawake (TWFA), Zena Chande (kushoto), na Katibu wake Mkuu Somoe Ng'itu.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF, Zena Chande ambaye ni Mhariri Msaidizi wa Michezo kazeti la HABARILEO akifuatilia mkutano huo.
Wawakilishi kutoka FIFA na CUF wakifuatilia mkutano huo.
Wallace Karia ni mmoja wa wagombea wa nafasi ya Urais.
Waziri Mwakyembe akizungumza na Wadhamini wa TFF, Joel Nkaya Bendera (kushoto) na Steven Mashishanga (kulia)
Ofisa wa Polisi akizungumza na wanahabari pamoja na wadau wa soka waliokuwa nje ya ukumbi wa mkutano na kuwataka waondoke eneo hilo.
Ofisa Usalama wa FIFA Tanzania, Inspekta Hashim Abdallah akiwaeleza jambo wanahabari.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment