Kaimu
Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(TBII-JNIA), Joseph Nyahende (wa pili kushoto) akitoa ufafanuzi wa
namna abiria wenye viza
wanavyohudumiwa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (mwenye miwani kifuani). Pembeni ya Waziri ni Katibu
Mkuu sekta ya Uchukuzi, Dr. Leonard Chamuriho na nyuma mwenye suti nyeusi
ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Salim Msangi.
Katibu
Mkuu wa chama cha madereva wa taxi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha
Julius Nyerere, Simon Mwampashi (kulia), akitoa maoni mbalimbali kwa Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa leo alipofanya
ziara JNIA.
Mkuu
wa Kitengo cha Idara ya Uhamiaji Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius
Nyerere, Flugence Andrew (kulia) akitoa maelezo ya utaratibu unaotumika
kulipia viza kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa,
leo alipofanya ziara kwenye jengo la abiria la kiwanja hicho.
Afisa
wa Benki ya NMB, Leah Rutayungurwa (aliyendani
ya dirisha) akimmsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof
Makame Mbarawa aliyetaka kujua muda anaohudumiwa abiria mmoja wakati akilipia
viza kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (TBII-JNIA).
Afisa
Forodha Msaidizi, Hezron Giso (kulia), akielezea shughuli anazozifanya ndani ya
Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (TBII-JNIA), kwa Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (mwenye miwani
kifuani), wakati wa ziara ya Waziri iliyofanyika leo.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akimsikiliza Kaimu
Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (TBII-JNIA),
mwenye kizibao akielezea jambo katika meza ya ukaguzi wa tiketi za abiria
wanaosafiri. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA), Salim Msangi.
***************
WAZIRI wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema ataunda timu ya
wataalmu kwa ajili ya kupitia mikataba ya wafanyabiashara katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa julius Nyerere (JNIA).
Ametoa
kauli hiyo baada ya kukagua huduma mbalimbali katika uwanja huo wa ndege ambapo
amesema, mikataba minne itaanza kupitiwa kwa kuwa inaonekana kuwa na kasoro.
"Nimeuliza
kidogo lakini inaonekana analipa kila baada ya mwezi, lakini mimi ninapokodi
nyumba nalipa kila baada ya mwaka, tuna changamoto kubwa ya mikataba hapa
uwanja wa ndege," amesema Profesa Mbarawa.
"Kuna
mikataba minne tayari nimeshaona ambayo tutayarisha timu ya wataalamu
watakaopitia upya, sio tu hii hata mingine ni lazima tuweke utaratibu mzuri
ambao serikali inapata fedha inayostahili na fedha hizo tukizipata tutaboresha
uwanja wa ndege wa hapa," amesema.
Katika
hatua nyingine, amesema pia uongozi wa uwanja huo wa ndege ni mzuri lakini
hauendi na inayotakiwa, kwani uongozi unaotakiwa ni wa watu wenye uzalendo wa
kukusanya kodi na pia kupeleka mbele uwanja huo.
Profesa
Mbarawa amesema, uongozi wa uwanja huo pia uhakikishe unaondoa malalamiko
yaliyopo ya abiria wanaoingia nchini kukaa muda mrefu katika kupata huduma.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment