Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Saimon Sirro, amefanya mabadiliko ya Kamanda wa Kikosi cha
Usalama Barabarani pamoja na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya.
Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa
Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Mohamed
Mpinga anaenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, na nafasi yake
inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus
Musilimu.
Aidha, Aliyekuwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya (DCP) Dhahiri Kidavashari amehamishiwa Makao
Makuu ya Upelelezi.
Uhamisho huo ni wa kawaida katika kuboresha
utendaji wa kazi za Polisi kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi
la Polisi.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment