UNAWEZA kumpachika jina la Malkia wa Sokwe Tanzania na hii ni kutokana na jinsi alivyokuwa mlezi wa wanyama hao ambao walikua katika tishio la kutoweka na kutokana na shughuli za kibinadamu. Anaandika Mroki Mroki wa TSN Digital.
Huyu si mwingine bali ni Katibu Muktasi aliyeamua kuzama katika utafiti wa wanyama pori hasa Sokwe na kuamua kusafiri kutoka nchini Uingereza mwaka 1960 akiwa na umri wa miaka 26 na kuamua kuingia hifadhi ya taifa ya gombe na kufanya utafiti juu ya maisha ya wanyama hao wenye hulka za kibinadamu.
Unapo wazungumzia Sokwe wa Gombe, katu huwezi kwenda mbali na jina la
Valerie Jane Morris-Goodall au kama alivyotambulika hapo mwanzo wakati wa ndoa yake ya awali kama Baroness Jane van Lawick-Goodall na sasa anatambulika kama Jane Goodall mzaliwa wa Uingereza aliyeishi nchini Tanzania kwa miaka takribani 57 akifanya utafiti.
Inaelezwa kuwa alipata kuwa Mke wa mmoja wa wabunge wa Bunge la Tanzania na Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa nchini, miaka ya nyuma, na mumewe huyo aliyetajwa kwa jina la Derek Bryceson.
Leo wakati Jane Goodall umri wake ni miaka 83, katika kutambua mchango wake hapa nchini katika uhifadhi wa Sokwe, Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania limeamua kumtunuku mama huyu rafiki kipenzi wa Sokwe wa Gombe, tuzo maalum ya kutambua mchango wake mkubwa katika eneo la utafiti wa sokwe hususan katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe.
Tuzo hiyo inayofahamika kama Sokwe Conservation Award imekabidhiwa kwake na Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe aliyekuwa mgeni rasmi katika tukio hilo.
Tuzo hiyo inayofahamika kama Sokwe Conservation Award imekabidhiwa kwake na Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe aliyekuwa mgeni rasmi katika tukio hilo.
Mbali na tuzo hiyo lakini pia TANAPA ilimzawadia zawadi ya kipekee ya kinyago nadhifu cha Sokwe ambacho mwenye alikiita Fifi. Akimaanisha Sokwe maarufu wa Gombe aliyeitwa Fifi.
Hawakuishia hapo lakini pia walimpa zawadi ya picha ya kuchorwa ya Sokwe aliye na mwanae. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Kama mwanamke wa kitanzania alikabidhiwa na zawadi ya Kitenge, hapa mama Mongela akimvisha kitenge hicho.
Dk Jane Goodall akiwa meza kuu na tuzo yake na zawadi zake nyingine. Mdoli wa sokwe anaekula ndizi ni moja ya vitu anavyovipenda sana na humkumbusha jinsi alivyokuwa akiwapa ndizi sokwe hao.
Mkurugenzi wa Shirika la
Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya utoaji tuzo kwa Dk Jane Goodall, jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Jenerali (Mstaafu) George Waitara akizungumza
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza wakati wa halfa hiyo ya utoaji tuzo.
Mabalozi kutoka nchi mbalimbali waliohudhuria.
baadhi ya wajumbe wa Bodi ya TANAPA na Wakuu wa mikoa ya Katavi na Kigoma wakifuatilia tukio hilo la heshima.
Baadhi ya waalikwa
Wajukuu wa Dk. Jane Goodall wakifuatilia.
Meza kuu katika utoaji tuzo hiyo.
Mtafiti wa Sokwe, Dk Jane Goodall akitoa maelezo ya picha za matukio mbalimbali yahusuyo tafiti zake za sokwe ndani na nje ya Tanzania
Mkurugenzi wa Utafiti wa Nyani kutoka Taasisi ya Jane Goodall Tanzania, Dk. Anthony Collins akitoa maelezo mbalimbali kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Jumanne Maghembe wakati akiangalia matukio mbalimbali ya picha za utafiti wa Dk Jane Goodall.
Mkurugenzi
wa Utafiti wa Nyani kutoka Taasisi ya Jane Goodall Tanzania, Dk.
Anthony Collins akitoa maelezo mbalimbali kwa Waziri wa Maliasili na
Utalii, Dk Jumanne Maghembe wakati akiangalia matukio mbalimbali ya
picha za utafiti wa Dk Jane Goodall.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment