Toyota VX lenye namba
za usajili T329 DGK alilokuwa akisafiria Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Ruvuma, Sikudhani Chikambo (picha ndogo) iliyopata ajali na kusababisha kifo cha mtu mmoja leo mchana eneo la Dumila, Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro.
MBUNGE wa
Viti Maalum mkoa wa Ruvuma CCM, Sikudhani Chikambo amenusurika kifo katika
ajali ya barabarani hii leo Dumila, Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro. Anaandika John Nditi-Morogoro.
Mbunge
huyo pamoja na watu wengine watano walikuwa wakisafiri kutoka Dodomna kwenda
jijini Dar es Salaam ndipo gari walilokuwa wakisafiria Toyota VX lenye namba
za usajili T329 DGK, kupasuka gurudumu
na kuacha njia na kupinduka na kusababisha kifo cha ndugu wa Mbunge huyo.
Akizungumza akiwa katika Hospitali ya Mkoa wa
Morogoro alikolazwa kwa matibabu alisema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wake
kuwepa shimo lakini kutokana na ukubwa wa shimo hilo gurudumu lilitumbukia na
kupasuka kisha gari kupoteza muelekeo na kupinduka mara tano.
“Dereva
alikuwa anakwepa shimo, lakini kutokana na ukubwa wa shimo tairi lika tumbukia
na kupasuka gari iliyumba na kupoteza mwelekeo …na kupinduka mara tano kabla ya
kusimama,”alisema Sikudhani.
Alisema
aliyepoteza maisha ni ndugu wa karibu wa kiume aliyekuwa akiishi Dodoma na
kufanyia kazi za ujenzi wa nyumba.
Alisema
baada ya ajali walikimbizwa Hospitali ya Kanisa Katoliki Dumila na baadae kuhamishiwa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Morogoro.
Wabunge
Mbalimbali wa mkoa wa Morogoro wakiongozwa na Mbunge wa Morogoro mjini, Abdulaziz
Abood, Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Omary Mgumba, Mbunge wa Mtera, Livingstone
Lusinde na Mbunge wa Viti Maalumu Vyuo
Vikuu, Dk Jasmine Tisekwa walimtembelea na kumjulia hali.
Dk Tisekwa
ndiye alimsaidia Mbunge mwenzake na majeruhi kuletwa hostitali kuu.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment