Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango,(kulia), akimkabidhi kadi ya uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, kupitia Mpango wa "Wote Scheme", kijana wa miaka 18, Msuya S. Mageta, kwenye banda la Mfuko huo kwenye jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, Viwanja vya Mwalimu Nyerere, maarufu Sabasaba ambako kunafanyika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam.
Waziri Dkt. Mpango, akimpongeza, Sukulu Mageta, mzazi wa Msuya Mageta, (katikati), kijana wa miaka 18 aliyeamua kujiunga na mpango wa Wote Scheme.
Meneja Elimu kwa Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Kwame Temu, (kushoto), akimkabidhi mkoba wenye vipeperushi vya taarifa za PPF, Waziri Dkt. Mpango.
Dkt. Philip Mpango, akikaribishwa na Meneja Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele, alipotembelea banda la Mfuko huo leo Julai 8, 2017.
Lulu Mengele akitoa maelezo mbele ya Dkt. Mpango kuhusu huduma zitolewazo na PPF
Dkt. Mpango akisikiliza kwa makini maelezo ya Meneja Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele
Lulu Mengele akitoa maelezo mbele ya Dkt. Mpango kuhusu huduma zitolewazo na PPF
Sukulu Mageta, mzazi wa Msuya Mageta, akieleza ni kwa nini aliamua kumuunga mkono kijana wake Msuya, kujiunga na PPF. Alisema, "Mimi kama mzazi uamuzi wa kijana wangu kujiunga na PPF, ni uamuzi sahihi na hii itanirahisishia hapo baadaye ambapo kwa mujibu wa maelezo tuliyopewa na maafisa wa PPF, mwanachama anaweza kupata mafao mbalimbali yakiwemo ya kujiendeleza kielimu, lakini pia bima ya afya na kijana wangu ndio kamaliza kidato cha sita na anahitaji kuendelea na masomo, kwa hiyo baadaye atafaidika ikiwa ni pamoja na kujiwekea akiba". Alisema Mageta
Waziri Dkt. Mpango, akishuhudia jinsi Katibu wake, Edwin Makamba, (wapili kulia), ambaye ni mwanachama wa PPF kupitia mpango wa Wote Scheme, akichangia kupitia simu yake ya mkononi. wengine pichani ni Meneja Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele, (kulia) na Meneja Elimu kwa Wanachama wa Mfuko huo, Kwame Temu. (kushoto).
**************
Waziri
Mpango leo Julai 8, 2017, alitembelea banda hilo na kuipongeza PPF kwa
uamuzi wake wa kuiunga mkono serikali katika jitihada zake za kujenga
uchumi wa viwanda.
PPF imeingia ubia na Jeshi la Magereza kukiboresha na
kuendesha kiwanda cha viatu Karanga kilichoko mjini Moshi. Hali
kadhalika, Mfuko huo kwa kushirikiana na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii,
NSSF, wameingia ubia katika mradi wa ujenzi wa kiwanda cha sukari huko
Mkulazi mkoani Morogoro na kiwanda kingine cha sukari Mbigiri pia kiko
mkoani Morogoro.
"Ninyi ni watu wazuri na niwapongeze kwa uamuzi wenu
mzuri wa kuiunga mkono serikali ya awamu yab tano ambayo tumejikita
katika kujenga uchumi wa viwanda ," Alisema Dkt. Mpango.
Alisema kwa
muda mrefu Mifuko ya Hifadhi ya jamii imewekeza kwenye majengo, lakini
niwahakikishie uwekezaji kwenye viwanda utatoa fursa nyingi kwa
watanzania, alisisitiza Dkt. Mpango.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment