Viongozi na wachezaji wa timu ya UMITASHUMTA Mkoa wa Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuibuka mabingwa wa michezo hiyo kitaifa mwaka huu 2017.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela
pamoja na Waziri wa Elimu Joyce Ndalichako wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mwanza.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela
pamoja na Waziri wa Elimu Joyce Ndalichako wakifungua shampeni huku
wakiipongeza mkoa wa Mwanza
********************
Na Alexander
Sanga,Mwanza
Mkoa wa Mwanza umeiibuka
bingwa wa jumla katika mashindano ya michezo ya shule ya msingi nchini kwa
mwaka 2017
Mwanza imetwa ubingwa
huo katika michezo hiyo iliyokuwa ikifanyika katika shule ya msingi ya Butimba
na chuo cha ualimu cha Butimba TTC mjini hapa
Katika riadha upande wa
wasichana mkoa wa Manyara ulishika
nafasi ya Tatu,Simiyu ikawa ya pili na Mwanza ilikuwa ya Kwanza.Upande wa
riadha wavulana mkoa wa Geita iliibuka na ushindi nafasi ya pili ilichukuliwa
na Shinyanga na mkoa wa Manyara uliambulia nafasi ya tatu.
Katika kombe la usafi
upande wa wavulana, Dodoma ilikuwa ya kwanza ikifuatiwa na Songwe kisha Mbeya ikiwa ya Tatu.
Kwa wasichana Manyara ilikuwa ya kwanza huku Dodoma
ilimaliza katika nafasi ya pili na
Kilmanjaro ikamaliza nafasi ya Tatu.
Kwenye mchezo wa Mpira
wa wavu kwa wavulana mkoa wa Dar-es-salaam ulitwa ubingwa,Mwanza ilimaliza
nafasi ya pili na Katavi ikawa nafasi ya Tatu.Upande wa wasichana Katavi ilitwa
ubingwa na nafasi ya pili ilichukuliwa na Mtwara huku Geita ilimaliza nafasi ya
Tatu.
Katika mchezo wa mpira
wa mikono,kwa wavulana Songwe ilitwa ubingwa,Mwanza ikamaliza nafasi ya pili na
Geita ilikuwa ya Tatu.kwa upande wa wasichana Mwanza ilitwaa ubingwa,Geita
ikawa ya pili na mara ilishika nafasi ya Tatu.
Katika soka maalumu kwa
wavulana Njombe ilitwaa ubingwa,Kagera ilishika nafasi ya pili na Dar-es-salaam
iliambulia nafasi ya tatu.
Katika soka la kawaida
wavulana,Mwanza ilitwaa ubingwa,Morogoro iliambulia nafasi ya pili na Mara
ikawa nafasi ya Tatu.
Katika mchezo wa
netiboli,Mwanza ilitwaa ubingwa,Geita ilishika nafasi ya pili na Arusha
waliambulia nafasi ya Tatu.
Waziri wa Elimu,
Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Joyce Ndalichako alisema serikali
itaendelea kuinua vipaji katika michezo na aliziomba Halmashauri zitenge bajeti
maalumu kwajili ya michezo
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment