Naibu Mhifadhi (Huduma za Shirika) wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Asangye Bangu (kulia), akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa TFF wa Maendeleo ya Soka (TFDF), Derek Murusuri, jijini Dar es Salaam leo.
Bangu alizitembelea ofisi za TFDF ili kujadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano kati ya Mamlaka yake na Mfuko huo. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi za TFDF zilizoko Mikocheni jijini Dar Es Salaam leo (28 June 2017).
Katika mazungumzo hayo, Bangu ameahidi kushirikiana na Mfuko huo katika kuendeleza soka la Tanzania.
Timu ya Taifa ya vijana walio chini ya miaka 20 (U-20), Ngorongoro Heroes, inatumia jina la Mamlaka hiyo ya Taifa ambayo pia ni mojawapo ya maajabu saba ya dunia.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment