Mkuu wa wilaya ya Mbogwe,Martha Mkupasi amewataka wananchi wa Mbogwe watoe ushirikiano wa kutosha kwa Mradi
Pendekezwa wa ujenzi wa Bomba la
Kusafirishia Mafuta Ghafi (EACOP)
linalotarajiwa kujengwa kutoka Ziwa Albert
kupitia Kabaale (Uganda)
hadi Rasi ya Chongoleani iliyo karibu na
Bandari ya Tanga.
Mkuu wa wilaya ameyasema hayo
alipofungua kikao cha maoni ya wadau
(scoping) kwa Wakuu wa Idara na watendaji wa kata wa Halmashauri ya wilaya ya Mbogwe kuhusu
Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii
(TAM) ya mradi wa EACOP.
Akiongea wakati wa ufunguzi bi Martha amesema mradi huo utaleta maendeleo kwa wanambogwe wote hivyo ni jukumu lao kuulinda .
Akiongea wakati wa ufunguzi bi Martha amesema mradi huo utaleta maendeleo kwa wanambogwe wote hivyo ni jukumu lao kuulinda .
Mradi wa Ujenzi wa Bomba la
Kusafirishia Mafuta Ghafi kutoka Uganda
(Ziwa Albert) hadi Tanzania (Tanga) lenye urefu wa kilometa 1445 linatarajiwa kupita
katika wilaya ya Mbogwe. Akiongea wakati
wa kikao hicho ,mwezeshaji kutoka kampuni ya JSB Envi-Dev Ltd Dr. Godfrey Kamukara ameelezea faida
zitakazopatikana kutokana na mradi huo zikiwemo upatikanaji wa ajira kwa wakazi
wa Mbogwe .
Hata hivyo alitahadharisha kuwa mradi huo unatarajiwa kusababisha mwingiliano wa makabila mbalimbali hivyo kuwataka watendaji hao wawaelimishe wananchi kujikinga na maradhi ikiwemo ugonjwa wa ukimwi.
Hata hivyo alitahadharisha kuwa mradi huo unatarajiwa kusababisha mwingiliano wa makabila mbalimbali hivyo kuwataka watendaji hao wawaelimishe wananchi kujikinga na maradhi ikiwemo ugonjwa wa ukimwi.
Dr.Kamukara amewataka
watendaji kuwaelimisha wananchi kuhusu mafuta ghafi ili wananchi wasitoboe
bomba wakidhani ni mafuta yanayofaa kwa matumizi . Alieleza kuwa mafuta ghafi
ni mafuta ambayo bado hayajasafishwa kwa matumizi ya kawaida.
Kampuni ya RSK ya
Uingereza na washirika wake kutoka
Uganda ( ECO partners ) na Tanzania ( JSB Envi-Dev Ltd) wameanza kazi ya Tathimini ya Athari kwa Mazingira na Jamii kwa kushirikisha jamii yote inayopitiwa na
mradi kwa kutoa maoni ya mambo muhimu ya kuzingatiwa wakati wa utekelezaji
wa mradi huo.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment