Na: Jovina Bujulu –
MAELEZO
SERIKALI mkoani
Iringa imesema hakuna njaa kwa sababu msimu wa mwaka 2015/2016 walizalisha tani
zaidi ya milioni 1.4 zikijumuisha mazao ya nafaka, mizizi na mazao jamii ya kunde.
Akizungumzia hali ya
upatikanaji wa chakula mkoani humo Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema
kuwa baadhi ya wananchi wengi wamejawa na tama ndiyo maana wanauza chakula
badala ya kuhifadhi kwa ajili ya matumizi ya familia zao.
“Kila kaya inatakiwa
kuhakikisha ina chakula cha kutosha badala ya kukiuza, na wataalam wa chakula
wataendelea kupita kila nyumba kuhimiza utuinzaji wa chakula sambamba na uwiano
wa mahitaji halisi,” alisema Mama Masenza.
Aliongeza kuwa kwa
sasa Mkoa huo una ziada ya mazao ya nafaka tani 756,369.92 na kunde tani
61,584.63.
Hata hivyo alitoa
wito kwa baadhi ya wananchi kuthamini familia zao kwa kuhifadhi chakula badala
ya kukiuza kwa tama zao za kupata fedha kirahisi.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment