Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye akitoa neno la ukaribisho kwa wadau wa Sekta Binafsi kwenye mkutano wa ndani ulioambatana na chakula cha jioni kilichoandaliwa na TPSF katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Dk. Reginald Mengi.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Dk. Reginald
Mengi akizungumza na wadau wa Sekta Binafsi katika mkutano ulioambatana
na hafla ya chakula cha jioni uliofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini
Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la
Biashara (TBNC), Mhandisi Raymond Mbilinyi.
WADAU
wa Sekta binafsi nchini Jumanne wiki hii, wamefanya mkutano ikiwa ni
sehemu ya maandalizi ya mkutano wao na serikali chini ya jukwaa la
Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) unaotarajiwa kufanyika Mei 6 mwaka
huu.
Mkutano huo wa ndani uliandaliwa na Taasisi ya Sekta binafsi nchini -
TPSF ulilenga kuwekana sawa kuhusu namna bora ya kuiwakilisha sekta
binafsi katika mkutano huo muhimu, ambao Mwenyekiti wake ni Rais wa
Jamhuri ya Tanzania Dr. John Pombe Magufuli.
Akiwakaribisha wadau wa Sekta Binafsi katika kikao hicho cha maandalizi
Mwenyekiti wa TPSF Dk. Reginald Mengi alisema Serikali na Sekta Binafsi
hawakomoani, ndio maana TPSF inahimiza wafanye kazi kwa pamoja ili
kulifikisha taifa kwenye uchumi wa viwanda
Dk Mengi pia alisema serikali na sekta binafsi wana malengo yanayofanana ya kutokomeza umaskini na kutengeneza ajira kwa wananchi, jambo ambalo linaweza kutekelezeka kwa urahisi iwapo kutakuwa na ushirikiano wa karibu baina ya serikali na Sekta Binafsi.
Katibu Mtendaji wa TNBC Mhandisi Raymond Mbilinyi alisema mkutano huo utakuwa ni fursa nzuri kwa serikali na sekta binafsi kubadilishana mawazo kuhusu wajibu wa kila upande katika kuboresha mazingira ya biashara na uzalishaji nchini ili kukuza uchumi wa nchi.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Roberto Jarrin akijitambulisha katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Dk. Reginald Mengi akiendelea na mazungumzo na wadau wa Sekta Binafsi kwenye mkutano huo ulioambatana na chakula cha jioni katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TBNC), Mhandisi Raymond Mbilinyi akifafanua jambo katika mkutano wa ndani ambao ni sehemu ya kujiandaa kukutana na serikali chini ya Baraza la Taifa la Biashara (TBNC) linalotarajiwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi Mei jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Dk. Reginald Mengi akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye wakati mkutano huo ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment