Wajumbe wa Kikosi cha Kitaifa
cha kunusuru ikolojia ya Mto Ruaha (kikundi namba 2) wakiwa katika picha ya
pamoja wakati wakisubiri kupanda boti ya upepo ili kutembelea eneo la bonde la
Ihefu lililoko Mbalari- Mkoani Mbeya kugagua ikolojia ya Bonde hilo.
Wajumbe wa Kikosi kazi wakiwa
ndani ya boti katikakti ya bonde la Ihefu wakiakagua ikolojia ya bonde hilo.
Kuanzia kulia ni Mkurugenzi Tume ya Umwagiliaji Injinia Seth Lusweme,
Mkurugenzi Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Richard Muyungi na Mkurugenzi wa
Bonde la Rufiji Idris Msuya.
Afisa Mkuu toka TANAPA Kanda
ya Arusha Vitalis Uruki akiongea na Wanahabari mara baada ya ziara ya kikosi
kazi katika bonde la Ihefu katika Wilaya ya Mbalari Mkoani Mbeya.
Na
Mwandishi Wetu
KIKOSI
cha Kitaifa cha kunusuru Ikolojia ya Mto Ruaha Mkuu, kilichoundwa na Makamu wa
Rais, Samia Suluhu Hassan kilichoko mkoani Mbeya, kimeendelea na ziara yake kwa
kutembelea skimu ya Mwendamtitu iliyopo wilayani Mbarali.
Kwa
mujibu wa taaifa ya Ofisi ya Makamu wa Rais kwa vyombo vya habari, katika ziara
hiyo, Kikosi kazi kiligundua jinsi ambavyo miundombinu ya skimu hiyo
inavyopoteza maji ambayo yalitakiwa kuingia Mto Ruaha.
Aidha,
pia kimegundua kuwa skimu hiyo imeanzishwa pasipo kufuata sheria za umwagiliaji
kwani haina kibali cha umwagiliaji wala kibali cha matumizi ya maji yanayoingia
katika mfereji wa skimu hiyo.
Wakizungumza
katika ziara hiyo, wajumbe wamesikitishwa na kitendo cha skimu hiyo cha kutumia
maji mengi pasipo kuwa na kibali chochote wala pasipokuwa na miundombinu ya
mifereji inayowezesha maji kurudi mto Ruaha Mkuu.
“Katika
skimu hii, maji yanatiririka bure na kwa aina hii ya umwagiliaji kamwe mto
Ruaha Mkuu hautapata maji, ila tutachukua hatua stahiki,” alisema mjumbe Seth
Luswema.
Kwa
upande wa wananchi wa eneo hilo wameiomba serikali iwasaidie kuwapatia elimu
jinsi ya kuendesha skimu hiyo na pia kuelekezwa jinsi ya kuweka miundombinu
rafiki kwa ajili ya kuokoa kiasi cha maji kinachopotea. Walisema wao hawana
elimu yoyote na hawajui kama wanakosea kwa jinsi wanavyoendesha skimu hiyo.
Kikosi
hicho bado kipo mkoani Mbeya wilayani Mbarali kwa ajili ya kuzungukia na
kukagua maeneo mbalimbali amabayo yanachangia maji kutokwenda Mto Ruaha Mkuu.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment