Waziri
Mkuu wa zamani na Mwanasiasa wa siku nyingi wa Kenya, Raila Amolo Odinga, au
maarufu kama anavyojulikana na wafuasi wake kama Agwambo, Tinga, Baba, RAO au Jakom, Odinga alikuwa Waziri Mkuu mwaka 2008 to
2013. Endapo atapitishwa na Muungano wa vyama vya upinzani Kenya (NASA) hii leo
atakuwa amegombea kwa mara ya nne mfululizo.
Aliyekuwa naibu wa Rais na kiongozi wa chama cha
Wiper, Kalonzo Musyoka amejilinganisha na Donald Trump na kuahidi ushindi
endapo atagombea uchaguzi ujao. Musyoka alipata kuwa makamu wa Rais wa Kenya
chini ya Utawala wa Rais Daniel Arap Moi 2008-2013
Musalia Mudavadi ni kiongozi wa Chama cha Amani
National Congress (ANC), na alipata kuwa Makamu wa Rais 2002 na Naibu Waziri Mkuu wa
Serikali ya Kenya kati ya 2008-2012.
Kiongozi wa Chama cha Mashinani (CCM) na Gavana wa zamani wa Gomet, Isaac Ruto nae ni mmoja wa wanasiasa wa Kenya walioonisha nia ya dhati kumpoka kiti rais Uhuru Kenyatta.
Kiongozi wa chama cha Ford Kenya Moses Wetangula, nae ni moja kati ya Wanachama wa tano wa Nasa wanaowania nafasi ya kuteuliwa kugombea Urais kupitia Muungano huo.
***********
ZIKIWA zimesalia siku 102 kufanyika kwa uchaguzi Mkuu
wa Rais, Magavana, Seneta, wabunge na madiwani nchini Kenya Muungano wa vyama
vya upinzani huenda wakatangaza mgombea wao hii leo.
Muungano huo wa vyama vya upinzani nchini Kenya una watu
watano mashuhuri wanaowania kuteuliwa na umoja huo kuchuana na Rais wa sasa wa
Kenya, Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa mwezi Agosti mwaka huu.
Taarifa kutoka ndani ya muungano wa vyama hivyo
vya upinzani nchini humo ujulikanao kama National Super Alliance, yaani NASA,
uilisema itatangaza mgombea wake wakati wowote.
Wagombea watano
walio ndani ya NASA, ni pamoja na mgombea Urais wa muda mrefu katika chaguzi za
Kenya Raila Odinga, ambaye anapewa nafasi kubwa ya kuteuliwa.
Wanasiasa
wengine walio ndani ya Nasa ni pamoja na Makamu wa Rais wa zamani Kalonzo Musyoka, Makamu
wa Rais wa zamani Musalia Mudavadi, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, Moses
Wetangula na Mwenyekiti wa zamani wa baraza la Magavana Isaac Ruto.
Ruto,
anayeongoza chama cha Chama cha Mashinani (CCM) alikuwa kwenye muungano wa
vyama vinavyomuunga mkono, Uhuru Kenyatta kabla ya kuhama na kuunda chama
chake.
Odinga ndiye
kiongozi wa chama cha ODM, ambacho kina wabunge wengi zaidi katika Bunge la
sasa.
Iwapo atachaguliwa kuwa mwaniaji wa Nasa, basi
itakuwa ni mara ya nne kwake yeye kuwania nafasi hiyo bila mafanikio ingawaje
anaamini kuwa alishinda uchaguzi wa mwaka 2007 ambapo Rais wakati huo, Mwai
Kibaki alitangazwa mshindi, na kuzua tafrani nchini Kenya ambapo watu zaidi ya
elfu moja waliuawa.
Huku hayo
yakijiri, wanasiasa wengi wanaendelea kupoteza viti vyao kwenye kura za maoni.
Wakenya kwenye mtandano wamekuwa wakiendesha
kampeni inayoitwa Opresheni Fagia Wote, ambapo baadhi ya maeneo ya uchaguzi yamewawafagia
Magavana, Seneta, wabunge na madiwani wote.
Kampeni ya
Fagia Wote inapania kuonyesha ghadhabu ya Wakenya kwa jinsi taifa hilo
limeendeshwa kwa miaka minne iliyopita. Kumezuka vurugu kwenye sehemu kadhaa
nchini na pia madai ya kuiba na kununua kura.
Askofu mmoja wa kike, Margaret
Wanjiru ambaye amewahi kuwa waziri, ambaye kwa sasa alikuwa anawania kuwa
Gavana mpya wa Nairobi, alilala kwenye seli ya Polisi alipokamatwa jana kwa
madai ya kuzua rabsha katika kituo cha uchaguzi.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment