HATIMAYE Muungano wa vyama vya
upinzani nchini Kenya National Super Alliance (NASA) umemteua aliyekuwa Waziri
Mkuu, Raila Omolo Odinga (pichani) kuwa mgombea wake katika uchaguzi mkuu utakaofanyika
Agosti mwaka huu.
Akizungumza baada ya kupewa
nafasi hiyo hii leo Odinga ambaye ni kiongozi wa chama cha ODM amesema kuwa
viongozi wa NASA wamempa heshima kubwa kuipeperusha bendera ya chama chao.
"Hii ni heshima kubwa sana
ambayo ndugu zangu wamenifanyia, kwa kuniweka nipeperushe bendera ya NASA.
Tumekuwa na vikao ambavyo vimechukua siku nyingi. Kila kitu tumeandika,
tumekubaliana ya kwanza serikali tutakayoiunda, ambayo ni serikali ya mseto
itakuwa ni serikali ya mpito," alisema Odinga.
Aliongeza
kwa kusema kuwa "Sisi tuko kama timu, yenye pembe tano (Pentagon),
wamenipa utepe wa nahodha, hiyo inaniunganisha mimi nao na Wakenya wote,
tutatembea pamoja bega kwa bega. Tunataka kubadilisha Kenya na kutekeleza ndoto
ya waanzilishi wa taifa letu".
Muundo wa Serikali ya NASA pindi ikiingia madarakani kuongoza Serikali ya Kenya
Akielezea vipaumbele vya serikali yake pindi akishika madaraka ya Kuiongoza Kenya kuwa ni kumaliza umasikini, kuimarisha afya, kuboresha uchumi, kubuni nafasi za kazi na kurejesha gharama ya elimu na maisha chini.
Odinga
pia ameahidi kuhakikisha walimu na madaktari,pamoja na wafanyakazi wengine
wanalipwa mishahara mizuri na kuahidi akishinda serikali yake itamaliza rushwa
serikalini.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment