Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi na Wadau wa mkoa wa Dodoma kwenye mkutano wa kazi ambapo Taarifa ya Awali ya mkoa wa Dodoma na utekelezaji wa uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma iliwasilishwa katika ukumbi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI.
Makamu wa Rais wa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi na Wadau wa mkoa wa Dodoma kwenye mkutano wa kazi ambapo Taarifa ya Awali ya mkoa wa Dodoma na utekelezaji wa uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma iliwasilishwa katika ukumbi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu
Hassan ameuagiza uongozi wa mkoa wa Dodoma uhakikishe unaondoa vitendo vya
ukiritimba kwa baadhi ya watendaji wa serikali ambavyo vinaweza kusababisha
ucheleweshaji au kukwamisha ujenzi wa miji mipya mikubwa mitano ya kisasa
katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dodoma.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu
Hassan ametoa kauli hiyo Machi 14,2017 wakati akifanya mazungumzo na viongozi
wa mkoa wa Dodoma baada ya kupokea taarifa ya Kikosi Kazi kilichoundwa na
serikali kwa ajili ya kuratibu shughuli mbalimbali za Serikali kuhamia Dodoma.
Makamu wa Rais Mhe Samia
Suluhu Hassan amesema ni muda muafaka sasa hivi kwa uongozi wa mkoa wa Dodoma
kujiimarisha na kujipanga ipasavyo katika kupokea wawekezaji wenye nia njema ya
kuwekeza kwenye sekta mbalimbali mkoani humo hasa wakati huu ambao serikali
inahamia Dodoma.
Ameonya kuwa wawekezaji
matapeli kamwe wasipewe nafasi ya kuwekeza Dodoma na ametaka uongozi wa mkoa wa
Dodoma kuwa makini makundi hayo ili wasije kuvuruga mipango ya serikali ya
kujenga Makao makuu ya kisasa katika Manispaa ya Dodoma.
Makamu wa Rais pia ameuagiza
uongozi wa mkoa wa Dodoma kulinda na kuendeleza maeneo yote yenye uoto wa asili
ili yasije yakaharibiwa kutokana na uwekezaji utakaofanyika mkoani humo.
Amesema amefurahishwa na kasi
ya uongozi wa mkoa wa Dodoma jinsi unavyojipanga katika kuhakikisha azma ya
serikali ya kuhamia Dodoma inafanikiwa kwa haraka ikiwemo utengaji wa maeneo
kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda na huduma za kijamii.
Kuhusu maeneo ya
wafanyabiashara wadogo, Makamu wa Rais,Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi
wa mkoa wa Dodoma wahakikishe wanatenga haraka maeneo maaluma kwa ajili ya
wafanyabiashara wadogo ili nao waweza kunufaika na mpango wa Serikali kuhamia
mkoani Dodoma.
“Ni muhimu maeneo yote
yatakayotengwa kwa ajili wafanyabiashara wadogo yawe huduma zote za
msingi ili kusaidia wafanyabiashara hao waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi
“Amesisitiza Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais Samia Suluhu
Hassan amesisitiza kuwa ni muhimu kwa uongozi wa mkoa wa Dodoma kuwashirikisha
viongozi wa wafanyabishara wadogo kuhusu maeneo yatakayotengwa ili kuondoa
malalamiko kutoka kwa wafanyabishara hao kupewa maeneo yasiyofaa wa ajili ya
shughuli zao.
Awali kabla ya kumkaribisha
Makamu wa Rais kuzungumza na viongozi wa mkoa wa Dodoma, Mkuu wa Dodoma Jordan
Rugimbana alimweleza Makamu wa Rais mipango na mikakati ya mkoa huo kuhusu azma
ya serikali ya kuhamia Dodoma ikiwemo uimarisha wa huduma za msingi ikiwemo
afya, miundombinu, maji na elimu.
Mkuu huyo wa mkoa wa Dodoma
Jordan Rugimbana amesema mpaka sasa kazi ya kuainisha maeneo mbalimbali kwa
ajili ya uwekezaji, makazi na mahali ambapo ofisi za serikali na za mabalozi
zitajengwa umeshakamilika.
Amesema uongozi wa mkoa wa
Dodoma utaendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali za serikali, mashirika ya
kimataifa na mabalozi ili kuhakikisha maeneo yaliyotengwa yanaendelezwa
haraka.
Ameeleza kuwa ujenzi wa miji
Mitano mikubwa mkoani Dodoma na ujio wa wawekezaji mbalimbali utaufanya mkoa
huo kuwa na uhitaji nishati ya umeme ya uhakika hivyo amehimiza ujenzi wa bomba
la gesi asili kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma ukafanyika haraka.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment