Wema Sepetu alipowasili Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam hii leo.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisitu jijini Dar es Salaam
imeahirisha kesi ya kukutwa na dawa za kulevya inayomkabili Miss Tanzania 2006,
Wema Sepetu pamoja na wenzake wawili hadi Aprili 11 mwaka huu.
Akitoa uamuzi huo leo Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas
Simba ameahirisha kesi hiyo kutokana na ombi lililowasilishwa na wakili wa
serikali, Costantine Kakula aliyeiambia Mahakama hiyo kuwa upelelezi wa kesi
hiyo bado haujakamilika ila upo katika hatua za mwisho.
Wema Sepetu ambaye pia ni Mwigizaji wa Filamu za
bongo maarufu kama ‘Bongo movie’ anakabiliwa na kesi hiyo yeye na wenzake
wengine wawili ambao ni mfanyakazi wake wa ndani Angelina Msigwa (21) na
mkulima Matrida Abas (16), ambao wote waliwakilishwa na Wakili Hekima Mwesigwa.
Watuhumiwa hao watatu wanadaiwa walitenda kosa
hilo Februari 4, mwaka huu nyumbani kwao Kunduchi Ununio jijini Dar es Salaam.
Ilidaiwa kuwa, siku hiyo walikutwa wakiwa na
msokoto mmoja na vipisi viwili vya bangi vya gramu 1.80 ambavyo ni dawa za
kulevya.
Washitakiwa wote wako nje kwa dhamana baada ya
kutimiza masharti ya kila mshitakiwa kuwa na wadhamini wawili, ambao watasaini
kila mmoja bondi ya Sh milioni tano.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment