Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wananchi
waliokumbwa na mafuriko katika maeneo ya Mnyamani na Tabata Kando
Kando ya Bonde la Mto Msmbazi kutokana mvua zinazoendelea kunyesha
katika jiji la Dar es Salaam.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo akitoa neno kwa
wananchi walifikwa na mafuriko katika eneo la myanyamani kando kando ya
bonde la Mto Msimbazi leo jijini Dar es Salaam.
************
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Pau Makonda amesema
nyumba 36 zilizojengwa kando kando ya Mto Msimbazi zianatakiwa kuvunjwa
kesho kutokana nyumba hizo zilishakuwa zimelipwa katika mafuriko
yaliyopita.
Akizungumza na wananchi waliopata
mafuriko jana, Makonda amesema watu walipewa viwanja mabwepande
waishindwa kuvunja ili waweze kupangisha kutokana na kuwa na akili
nyingi lakini dawa yake ni kesho kuzivunja.
Makonda
amesema kuwa kuna mpango wa kupata fedha kutoka benki ya dunia
zitapanua mto ambazo serikali ya Tanzania italipa fedha hizo na kuongeza
kuwa watu ambao wamejenga kandokando ya mto msimbazi.
Amesema
kuwa wakati wa matatizo ya mafuriko wanajitokeza kwa wingi lakini
mikutano ya kawaida mahudhurio hafifu hali hii lazima watanzania
tuondokane.
Aidha amesema kuwa serikali
inapoteza fedha nyngi kwa ajili ya kusaidia watu wenye maafa bila kujua
fedhahizo ni za kodi ambazo zinatakiwa zifanye shughuli za maendeleo
bila kujali watu wanaona fedha hizo zinatolewa mbinguni ambapo ni
ndoto.
Makonda amesema kuwa watu wanaojenga
nyumba kuanzia msingi wanaonekana lakini wananchi wanashindwa kusema
mpaka mafuriko yanaingia ndani ndio wanajua mafara ya nyumba kujenga
katika mkondo wa mto.
Mkuu wa Mkoa huyo amesema
kuna watu watafidia wale watu ambao kweli wanatakiwa kufidiwa na sio
wale waliohamishwa wakarudi tena .
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Mkoa wakiangalia eneo la Mnyamani na Tabata jinsi
lilivyoathirika na mafuriko ya jana.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akivuka katika kivuko cha
watembea kwa miguu kwenda kuangalia wananchi walioadhirika na mafuriko
leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akisaidiwa na kuvuka kuwenda
upande wapili katika eneo la Mnyamani na Tabata kando kando ya Bonde la
Mto Msimbazi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Mkoa wakiangalia eneo la Mnyamani na Tabata jinsi
lilivyoathirika na mafuriko ya jana.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment