Na Mwandishi Wetu
Mwanasiasa mkongwe Kingunge Ngombale Mwiru amefariki usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili (MHN), mtoto wake wa kiume, Kinje Ngombale amethibitisha.
Kinje hakutoa taarifa zaidi juu ya kifo cha mkongwe wa siasa hapa nchini, ila HabariLeo itakuletea taarifa kadiri zinavyopatikana.
Kingunge, aliyezaliwa mwaka 1930, ni miongoni mwa waasisi wa TANU na baadaye Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho alikitumikia hadi mwaka 2015 alipoamua kuunga mkono upinzani.
Alilazwa hospitalini hapo kwa muda mrefu akitibiwa majeraha baada ya kung’atwa na mbwa nyumbani kwake.
Kifo cha mwanasiasa huyo, kimetokea ikiwa ni takribani mwezi mmoja umepita baada ya mke wake, Peras Kingunge kuaga dunia.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment