Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Thursday 11 January 2018

KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI JOHN KIJAZI APOKEA KWA NIABA YA RAIS KANUNI ZA SHERIA YA MADINI NAMBA 7 YA MWAKA 2017

Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi akimpa muhtasari Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi kabla ya kumkabidhi vitabu vya Kanuni za sheria ya Madini namba 7 ya mwaka 2017 ambaye anapokea kwa niaba ya Rais Dkt John Pombe Magufuli aliyeagiza kuandaliwa kwa kanuni hizo ndani haraka ili sheria iweze kufanya kazi. Hafla hiyo ndogo, iliyohudhuriwa pia na Manaibu Waziri wa Madini, Doto Biteko na  pamoja na Katibu Mkuu  wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, imefanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi 11, 2018
Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi akimsikiliza  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi baada ya  ya kumkabidhi vitabu vya  Kanuni za sheria ya Madini namba 7 ya mwaka 2017 ambaye anapokea kwa niaba ya Rais Dkt John Pombe Magufuli aliyeagiza kuandaliwa kwa kanuni hizo ndani haraka ili sheria iweze kufanya kazi. Hafla hiyo ndogo, iliyohudhuriwa pia na Manaibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo na Doto Biteko na  pamoja na Katibu Mkuu  wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, imefanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi 11, 2018
Kitabu cha Kanuni za sheria ya Madini namba 7 ya mwaka 2017
Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi akimkabidhi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi  vitabu vya Kanuni za sheria ya Madini namba 7 ya mwaka 2017 ambaye anapokea kwa niaba ya Rais Dkt John Pombe Magufuli aliyeagiza kuandaliwa kwa kanuni hizo ndani haraka ili sheria iweze kufanya kazi. Hafla hiyo ndogo, iliyohudhuriwa pia na Manaibu Waziri wa Madini, Doto Biteko na  pamoja na Katibu Mkuu  wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, imefanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi 11, 2018.
 Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi  na Manaibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo na Mhe. Doto Biteko, pamoja na Katibu Mkuu  wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, wakiwa na vitabu vya  Kanuni za sheria ya Madini namba 7 ya mwaka 2017 baada ya  Balozi Kijazi kuvipokea kwa niaba ya Rais Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi 11, 2018.
Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi  akimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango kitabu cha Kanuni za sheria ya Madini namba 7 ya mwaka 2017 baada ya  Balozi Kijazi kuvipokea kwa niaba ya Rais Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi 11, 2018. Wengine ni Manaibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na Doto Biteko, pamoja na Katibu Mkuu  wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment