Jumla ya skauti wapatao 200 kutoka jimbo la Hamshire
Uingereza wapo nchini Tanzania kwa ziara ya kazi za jamii pamoja na skauti
wenzao wa Tanzania.
Skauti hao wamekuja nchini kwa ajili ya kufanya kazi za
jamii ambapo wamejitolea kukarabati Kambi kuu ya Mafunzo ya Skauti iitwayo
Bahati ambayo ipo mkoani Morogoro nje kidogo ya mji huo.
Ziara hiyo ambayo
itachukua zaidi ya mwezi mmoja kukarabati eneo hilo la kambi, na baada
ya hapo watatembelea maeneo mengine ya Kilosa, Ifakara, na Mikumi kabla ya
kurejea nchini kwao Uingereza.
Kazi za kujitolea kwa vijana Skauti ni mojawapo ya
shughuli zao za kila siku kusaidia watu siku zote kama Kanuni za Skauti
zinavyosema.
Hii ni mara ya kwanza kwa kundi kubwa la Skauti kutoka
Uingereza kutembelea Tanzania.
Wakiwa nchini Tanzania skauti hao kutoka nje
wanashirikiana na wenyeji wao Chama cha Skauti Tanzania, kutoka Makao Makuu D’salaam
na wengine wa mkoani Morogoro.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment