Raisi wa Mahakama akitambulisha Jaji Matusse kwa Raisi
was Guinea Bissau Ikulu. Kushoto wa pili ni Makamu wa Raisi wa Mahakama Jaji
Ben Kioko.
******************
|
Rais
wa Jamhuri ya Guinea Bissau Mheshimiwa Jose Mario Vaz ameahidi kuwa,
nchi yake itaridhia itifaki iliyoanzisha mahakama ya Afrika ya haki za
binadamu na watu (AfCHPR) mapema iwezekanavyo .
Akizungumza
na ujumbe wa mahakama hiyo ulioko katika ziara ya kikazi nchini Guinea
Bissau, Rais Vaz alisema hatua hiyo inatokana na ukweli kwamba
Guinea Bissau ilikuwa miongoni mwa nchi za mwanzo za umoja wa Afrika
kutia saini itifaki iliyoanzisha AfCHPR mwaka 1998.
Katika
mazungumzo yake na ujumbe huo ulioongozwa na rais wa AfCHPR mheshimiwa
Jaji Sylvain Ore kiongozi huyo wa Guinea Bissau alielezea kuridhishwa
kwake na madhumuni ya kuanzishwa kwa mahakama ya Afrika ya haki za
binadamu na watu na kuongeza kuwa masuala ya haki za binadamu yana
umuhimu mkubwa katika kufikiwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika
nchi za Afrika na kuwaondoa wananchi wake katika lindi
la umaskini na ufukara.
“Ahadi yangu ni kuhakikisha kuwepo kwa haki za binadamu katika nchi yangu” alisisitiza Rais Vaz.
Ujumbe
wa AfCHPR pia ulikutana na waziri mkuu wa Guinea Bissau Mheshimiwa
Umario Sissoco Embalo ambaye alisema mamlaka husika za nchi yake
zitaandaa
nyaraka zinazohitajika ili kuzipeleka katika bunge la taifa nchini humo
kwa lengo la kuridhia itifaki iliyoanzisha mahakama ya Afrika ya haki
za binadamu na watu.
“Mimi
ni muumini mkubwa wa umajumui wa Afrika (Pan-Africanism) na nitafanya
kila linalowezekana kuimarisha taasisi za umoja wa afrika” alisisitiza
waziri mkuu huyo.
Rais
wa AfCHPR jaji Ore na ujumbe wake ambao umejumuisha Makamu wa rais wa
mahakama hiyo Mheshimiwa Jaji Ben Kioko, Mheshimwa Jaji Angelo Matusse
na baadhi ya maafisa wa ofisi ya msajili wa AfCHPR pia ulikutana na
Jaji Mkuu, waziri wa masuala ya jamii na pia kamisheni ya haki za
binadamu ya Guinea Bissau.
Jaji
Ore alisema ilikufanikisha malengo ya mahakama na pia kuimarisha mfumo
wa haki za binadamu barani Afrika nchi nyingi za umoja wa afrika hazina
budi kuridhia itifaki iliyounda AfCHPR kwa mujibu wa kifungu cha 34(6)
na kutoa tako rasmi la kutambua na kukubali a mamlaka ya mahakama kuweza
kupokea kesi za watu binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs)
Hadi sasa ni Nchi 30 tu kati ya nchi 55 wanachama wa AU ndio zimeridhia itifaki husika.
AfCHPR
yenye makao yake makuu jijini Arusha iko nchini Guinea Bissau kwa
ziara ya kikazi ya siku 2 ili kukutana na viongozi na wadau mbalimbali
kwa lengo la kuitangaza mahakama hiyo.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment