Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiongea na wakurugenzi wa
Idara na vitengo vinavyojitegemea kuhusu mikakati ya utendaji kazi kwa mwaka
2018 moja ya mkakati huo ukiwa ni kuendelea kutoa huduma bora za matibabu kwa
kiwango cha kimataifa katika kikao cha
kwanza cha Menejimenti kilichofanyika
hivi karibuni. Kulia ni Mwanasheria wa Taasisi hiyo Maulid Kikondo.
Wakurugenzi wa Idara na vitengo vinavyojitegemea
vya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi (hayupo pichani) alielezea kazi zilizofanyika
katika Taasisi hiyo kwa mwaka 2017 katika
kikao cha kwanza cha Menejimenti kilichofanyika
hivi karibuni. Jumla ya wagonjwa 1025 walifanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na bila
kufungua kwa mwaka 2017 na hivyo Taasisi kuokoa zaidi ya bilioni 29 ambazo Serikali ingezilipa
kama wagonjwa hawa wangefanyiwa upasuaji wa moyo nje ya nchi.
Kikao cha kwanza cha Manejimenti cha Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa
mwaka 2018 kikiendelea.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Magonjwa ya Moyo wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akisoma taarifa za utendaji kazi wa idara yake kwa
kipindi cha miezi mitatu katika kikao cha kwanza cha Menejimentikwa mwaka 2018 kilichofanyika
hivi karibuni.
Picha na JKCI
******************
Na Mwandishi Wetu,
UONGOZI wa Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) umewaahidi watanzania kuendelea kutoa huduma bora
za matibabu kwa kiwango cha kimataifa kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa ya
moyo wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.
Ahadi hiyo
imetolewa hivi karibuni na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed
Janabi wakati akiongea na wakurugenzi wa Idara na vitengo vinavyojitegemea
katika kikao cha kwanza cha Menejimenti kwa mwaka 2018.
Prof. Janabi ambaye
pia ni Mwenyekiti wa kikao hicho alizitaja
ahadi zingine ni pamoja na kuendeea kupunguza kupeleka wagonja nje ya nchi,
kupunguza gharama za tiba, kuongeza idadi ya huduma, kuboresha usafi katika
Hospitali na kuendelea kushirikiana na
wananchi.
Mwenyekiti huyo
alisema kwa mwaka 2018 wamejipanga kutoa
huduma kwa wagonjwa wengi zaidi ukilinganisha na mwaka jana ambapo jumla ya
wagonjwa 64,093 walitibiwa katika Taasisi hiyo kati ya hao wagonjwa wa nje walikuwa
60796 na waliolazwa 3297.
“Malengo tuliyokuwa
nayo kwa mwaka huu wa 2018 ni kuona wagonjwa wengi zaidi ya hawa tuliowaona
mwaka 2017 katika kliniki zetu za kila siku. Taasisi imejipanga kufanya
upasuaji wa kufungua kifua kwa wagonjwa 400 na bila kufungua kifua kwa wagonjwa
1000.Tunatarajia kuwa na kambi maalum za upasuaji wa moyo zisizozidi 15”.
“Mwezi huu tunatarajia kuwa na kambi mbili
zote ni za upasuaji wa bila kufungua kifua. Tunaanza na kambi ya watu wazima kwa kushirikiana na Taasisi ya Madaktari
Afrika ya nchini Marekani. Mwisho wa mwezi tutakuwa na kambi ya watoto kwa kushirikiana
na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart-SACH) ya nchini Israel”,
alisema.
Kwa upande wa
viongozi waliohudhuria mkutano huo Prof. Janabi aliwataka kuwasimamia wafanyakazi wanaowaongoza ili waweze kufanya
kazi zao kwa ufanisi na uweledi huku
wakifuata maadili ya watumishi wa Umma hii itawafanya wananchi waweze kupata
huduma bora zaidi.
Nao viongozi waliohudhuria
mkutano huo walisema kuwa watahakikisha wanafanya kazi zao kwa kujituma, kufuata
kanuni za kazi na kuwasimamia wafanyakazi
wanaowaongoza ili wananchi waweze kunufaika na matibabu ya moyo yanayotolewa
katika Taasisi hiyo.
Kwa mwaka 2017
jumla ya wagonjwa 1025 walifanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na bila
kufungua kifua katika Taasisi hiyo ambapo
zaidi ya bilioni 29 (Tshs. 29,725,000,000/=) ziliweza kuokolewa kama
wagonjwa hao wangetibiwa nje ya nchi.
Gharama za mgonjwa mmoja anayetibiwa nje ya nchi ugonjwa wa moyo ni zaidi ya
milioni 29.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment