Waumini wa Dini ya Kiislamu Mkoani Dodoma
wakishirki katika Swala ya Eid El Hajj, iliyoswaliwa kimkoa katika Msikiti wa
Gaddafi Mjini Dodoma jana ambapo pamoja na mambo mengine waislamu waliaswa
kudumisha amani na utulivu vilivyopo nchi na si kuleta machafuko. (Picha na
Mroki Mroki).
Waumini wa Dini ya Kiislamu Mkoani Dodoma
wakishirki katika Swala ya Eid El Hajj, iliyoswaliwa kimkoa katika Msikiti wa
Gaddafi Mjini Dodoma jana ambapo pamoja na mambo mengine waislamu waliaswa
kudumisha amani na utulivu vilivyopo nchi na si kuleta machafuko.
WATANZANIA wameaswa kuilinda na kudumisha amani
iliyopo nchini na kamwe wasithubutu kushawishiwa na watu kuivuruga kwa namna
yeyote ile. Anaandika Mroki Mroki-DAILY NEWS Digital.
Kauli hiyo imetolewa na Shehe na Kadhi wa
Mkoa wa Dodoma, Mustapha Shaaban wakati akitoa mawaidha baada ya swala ya Eid
El Hajj iliyoswaliwa kimkoa katika Msikiti Mkuu wa Gaddafi mjini Dodoma jana.
Shehe Shaaban alisema Tanzania kama mataifa
mengi ya afrika yaliasisiwa na viongozi wetu kwa njia ya amani lakini hadi sasa
mataifa mengi yameshavuruga amani yao na wanaishi maisha ya mashaka, hivyo
alisema Watanzania hawanabudi kujivunia hali ya amani iliyopo pasipo kuivuruga. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
“Urithi wetu ni amani na utulivu nan i urithi wa
umma wa waislamu dunia nzima hivyo hatuna budi kuendeleza na kudumisha upendo,
amani na mashikamano katika familia zetu, jamii na hata kwa taifa kwa ujumla,
kama ambavyo Mtume wetu, Muhamad (S.AW) alituhusia kufanya katika swala yake ya
mwisho ya Hijja,” alisema Shehe Shaaban.
Aidha alisema amani ya nchi yetu na Afrika ni
amani yenye historia kutoka kwa waasisi wa mataifa yetu akiwataja, Mwl. Julius
Nyerere, Nelson Mandela, Kwame Nkruma, Mohamad Gaddafi, Jomo Kenyatta na
wengine wengi.
Akitolea mfano wan chi ya Libya, Shehe Shaaban,
alisema taifa hilo lilikuwa ni lenye amani na utajiri mkubwa Afrika lakini
kutokana na kukubali chokochoko toka mataifa mengine waliamua kuvuruga amani
yao na sasa wapo katika hali mbaya ya kiuchumi.
Katika hatua nyingine, Shehe Shaaban amewaasa
wakazui wa mkoa wa Dodoma kutitumia fursa ya ujio wa serikali na viongozi wake
mjini Dodoma katika kujipatia maendeleo.
Alisema Maendeleo ya wana Dodoma hayanabudi
kuletwa na wenyeji wenyewe kwanza na wasisubiri wageni ndio walete maendeleo.
Alizitaka taasisi za dini, mashirika na taasisi
mbalimbali za mkoani Dodoma kuwekeza katika maeneo mbalimbali yakiwepo ya
elimu, afya na viwanda ili kuleta maendeleo mkoani humo.
Waumini wa Dini ya Kiislamu Mkoani Dodoma
wakishirki katika Swala ya Eid El Hajj, iliyoswaliwa kimkoa katika Msikiti wa
Gaddafi Mjini Dodoma jana ambapo pamoja na mambo mengine waislamu waliaswa
kudumisha amani na utulivu vilivyopo nchi na si kuleta machafuko.
Waumini
wa Dini ya Kiislamu walioshiriki katika Swala ya Eid El Hajj, iliyoswaliwa
kimkoa katika Msikiti wa Gaddafi Mjini Dodoma jana wakisikiliza mawaidha kutoka
kwa Shehe na Kadhi wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Shabaan (hayupo pichani)
ambaye aliwaasa waislamu na watanzania wote kudumisha amani na utulivu
vilivyopo nchi na si kuleta machafuko.
Waumini wakiingia na kutoa zaka
Wasichana
Waumini wa Dini ya Kiislamu wakiondoka katika viwanja vya Msikiti wa Gaddafi
mjini Dodoma baada ya kushiriki Swala ya Eid El Hajj, iliyoswaliwa kimkoa
katika Msikiti wa Gaddafi leo.
waumini wakipiga picha na Shekhe wa Mkoa wa Dodoma.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment