Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir amezipa miezi sita taasisi zilizoshindwa kusafirisha mahujaji kuhakikisha zinarudisha fedha zilizochukua toka kwa mahujaji takribani 100. Anaandika Katuma Masamba.
Ametoa kauli hiyo, leo wakati wa baraza la Eid Al Hajj lililofanyika Masjid Taqwa, Ilala Bungoni jijini Dar es Salaam ambalo pia limehudhuriwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi.
Mufti pia amesema taasisi ambazo zina mapungufu zitafutiwa usajili wake ili kulinda haki za waislamu.

Taasisi zilizoshindwa kusafirisha mahujaji ni Taiba Hajj & Umrah social service Trust na Jamarat Hajj & Umrah Travellers.
Naye Dk Mwinyi alitaka kuwepo na utaratibu wa kuzichunguza taasisi zilizo chini ya Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) ili kuzuia mambo kama hayo yasitokee.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment