Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani limekusanya Sh milioni 319 kutokana na faini za makosa mbalimbali barabarani.
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro amesema faini zimekusanywa kutokana na makosa 10, 645 yaliyokamatwa kuanzia Aprili 13 hadi 18, jijini hapa.
Amesema magari yaliyokamatwa ni pamoja na magari binafsi, maroli, daladala na pikipiki ambapo baada ya kukaguliwa yalipigwa faini zilizowesha kupatikana,kwa Sh 319, 350,000.
"Makosa haya yamekamatwa kwa muda mfupi sana, ni vizuri madereva na waendesha pikipiki wakatii sheria za usalama barabarani bila shuruti, hata sisi hatupendi kuina fedha hizi zinatolewa na wananchi wakati zingeweza kuwasaidia katika shughuli zao za kjmaendeleo," amesema Kamishna Sirro wakati akizungumza na waandishibwabhabari leo.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment