Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji
Na Mroki Mroki, Dodoma
JESHI la Polisi Mkoani Dodoma
linamtaka dereva wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliyetajwa kwa
jina moja la Adam,pamoja na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji kujitokeza na kufika Polisi Dodoma kwa
mahojiano.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,
SACP Gilles Muroto amesema dereva huyo anatakiwa kufika katika ofisi yake bila
kukosa au Makau Makuu ya Polisi jijini
Dar es Salaam ili aweze kutoa maelezo yake kuhusiana na tukio hilo.
“Jeshi la Polisi linamataka
dereva wa Tundu Lissu aitwae Adam ambaye alikuwa nae siku ya tukio, afike kwa
mahojiano kuhusiana na tukio hilo kwakuwa ndiye aliyekuwa pamoja na majeruhi
wakati wa tukio,”alisema Muroto.
Polisi pia limemtaka Katibu
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Vicent Mashinji kufika
kituo cha Polisi Dodoma au katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI),
Dar es Salaam kwa mahojiano.
Aidha Polisi mkoa wa Dodoma
linayashikilia magari nane aina ya Nissan pamoja na madereva wake kwa mahojiano
kuhusiana na magari hayo kuhisiwa kuhusika katika tukio la shambulizi la Mbunge
wa Singida, Tundu Lissu.
Aidha amesema Jeshi la Polisi
bado linaendelea na msako mkali wa watuhumiwa waliohusika katika tukio la
kumshambulia Mbunge Tundu Lissu nyumbani kwake.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment