Miongoni mwa Taaisi ambazo zimeshiriki maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam mwaka huu ni Taasisi ya Ujenzi wa Nyumba za Watumishi wa Umma (WHC) ambayo ipo katika Banda la Jakaya Kikwete. Leo hii katika kilele cha Siku kuu ya Sabasaba, Ofisa Mtendaji Mkuu wa WHC, Dk Fred Msemwa aliongoza timu ya watumishi wa taasisi hiyo kusikiliza wananchi mbalimbali waliotembelea banda hilo kwa lengo la kujua nini WHC inakifanya katika kuwapa wananchi hasa watumishi wa umma makazi bora na salama.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa WHC, Dk Fred Msemwa akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Taasisi hiyo waliokuwa wakihudumia wananchi waliotembelea Banda lao hii leo. Kulia ni Ofisa Mauzo, Irene Kasanda na kushoto ni Ofisa Uhusiano na Mauzo, Marijane Makawia.
TAASISI ya Ujenzi wa Nyumba za Watumishi wa Umma (WHC) imesema imejipanga kuwawezesha watumishi wa umma hasa kada ya chini na kada ya kati kumiliki nyumba kwa gharama nafuu. Anaandika Katuma Masamba.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa WHC, Dk Fred Msemwa akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Taasisi hiyo waliokuwa wakihudumia wananchi waliotembelea Banda lao hii leo. Kulia ni Ofisa Mauzo, Irene Kasanda na kushoto ni Ofisa Uhusiano na Mauzo, Marijane Makawia.
Naibu
Waziri, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk.Angelina
Mabula akipata maelezo ya miradi mbalimbali inayotekelezwa na Watumishi
Housing kutoka Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko Bwana Raphael
Mwabuponde alipotembelea banda lao katika maonesho ya kibiashara ya
sabasaba.
Kulia ni Ofisa Mauzo, Irene Kasanda na kushoto ni Ofisa Uhusiano na Mauzo, Marijane Makawia wakihudumia wananchi mbalimbali waliotembelea banda hilo hii leo./Picha: Mroki MrokiTAASISI ya Ujenzi wa Nyumba za Watumishi wa Umma (WHC) imesema imejipanga kuwawezesha watumishi wa umma hasa kada ya chini na kada ya kati kumiliki nyumba kwa gharama nafuu. Anaandika Katuma Masamba.
Ofisa Mtendaji Mkuu, Dk Fred Msemwa ameyasema hayo leo
katika maonesho ya 41 ya kimataifa ya biashara Dar es Salaan (DITF)
maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Julius Nyerere,
barabara ya Kilwa.
Amesema wamepanga kuwawezesha watumishi wa umma kummiliki
nyumba hizo kupitia mpango wa mpangaji mnunuzi ambao mtumishi anaweza
kununua nyumba kwa mtindo wa kuanza kuwa mpangaji na hatimaye kuwa
mmiliki.
"Tumekuja na mpango wa mpangaji mnunuzi, mtumishi badala ya
kwenda kupanga nyumba ya kawaida na wakati huo anasubiri kujenga,
anaweza kuja kwetu na fedha ambayo angetumia kupanga kwingine, ndio
anatumia kupanga kwetu hadi mwisho nyumba inakuwa mali yake," amesema Dk
Msemwa.
Aidha, amesema wameboresha huduma na kufanya ubunifu ili kuhakikisha Watanzania wanapata makazi bora kwa gharama nafuu.
Naye, Ofisa Mahusiano na Masoko wa WHC, Maryjane Makawia
amesema, kwa sasa wanatekeleza mradi wa makazi mkoani Dodoma ambao
utawawezesha watumishibwa umma wengi kumiliki nyumba.
Amesema mradi huo utahusisha ujenzi wa nyumba 460 ambapo awamu ya kwanza zitajengwa nyumba 159.
Maryjane pia ameongeza kuwa, kipindi cha nyuma Watanzania
waishio nje ya nchi walikuwa wanakosa fursa ya kumiliki nyumba nchini
lakini kwa sasa taasisi hiyo imekuja na mpango wa kuwawezesha Diaspora
kumiliki nyumba nchini.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment