Kikosi cha TPB Bank FC kilichoiadhibu taswa FC 3-2
Kikosi cha Taswa FC kilichokubali kichapo cha 3-2 kutoka kwa TPB Bank FC
***************
Na Mwandishi
wetu
Timu ya soka
ya TPB Bank FC imefanikiwa kulipiza kisasi kwa timu ya waandishi wa habari za
michezo nchini, Taswa FC baada ya kuifunga kwa mabao 3-2.
Mchezo huo
maalum, ulifanyika kwenye uwanja wa Shule ya Sheria (Law School) uliopo maeneo ya kituo cha mabasi cha
Mawasiliano na timu zote mbili zilishambauliana kwa zamu.
Katika
mchezo wa kwanza, Taswa FC iliifunga TPB Bank FC kwa mabao 4-0 katika mchezo
uliofanyika kwenye uwanja huo huo.
TPB Bank FC
ilitumia idadi pungufu ya wachezaji wa
Taswa FC kufunga mabao yote katika mchezo huo ambao pia ulikuwa wa maandalizi
kwa timu hiyo ya benki kuelekea katika mashindano ya soka ya taasisi za kibenki
yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni. Taswa FC ilianza mechi hiyo ikiwa na
wachezaji nane tu.
Bao la
kwanza la TPB Bank FC lilifungwa na nahodha wa timu hiyo, Baraka Kyomo katika dakika ya 10 ya mchezo baada ya kuwashinda kasi mabeki wa Taswa FC na
kufunga kirahisi.
Wakati Taswa FC ikijiuliza, Kyomo alifunga bao
la pili katika dakika ya 17 kabla ya Ojo Ajali kufunga la tatu katika dakika ya
35 ya mchezo.
Taswa FC
ilianza harakati za kusawazisha mabao hayo kuanzia kipindi cha pili baada ya
kutimia wachezaji wote 11. Bao la kwanza la Taswa FC lilifungwa na Fred Pastory
baada ya kupokea pasi safi ya Zahoro Mlanzi kabla ya Shedrack Kilasi kufunga la
pili kufutia mpira wa kona wa Juma Ramadhani.
Kiongozi wa
timu hiyo Chichi Banda alisema kuwa wamefuraishwa na ushindi huo na kuwaomba
Taswa FC kujipanga kwa ajili ya mchezo unaofuata.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment