Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala akizindua uwekaji
alama mifugo katika Kijiji cha Soweto wilayani Chunya mkoani Mbeya leo.
MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala amezindua uwekaji alama mifugo mkoani Mbeya.
MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala amezindua uwekaji alama mifugo mkoani Mbeya.
Makalla amefanya
uzinduzi huo leo katika Kijiji cha Soweto wilayani Chunya na kusema kuwa
uwekaji alama mifugo ni utekelezaji wa sheria ya mifugo namba 12 ya mwaka 2010.
Amewataka wafugaji wote 2,755
wa Wilayani Chunya kuhakikisha kuwa Ng’ombe 282,517 wanawasajili na kupiga
chapa.
Makalla amesema faida ya
kusajili na kuweka alama mifugo kuwa ni pamoja na kujua idadi ya mifugo, kuwa
na mipango ya matumizi bora ya ardhi ili kuepusha migogoro ya wakulima na
wafugaji.
Aidha amesema kuwa faida
nyingine ni kuzuia uingiaji mifugo kiholela na kuthibiti magonjwa ya mifugo.
Amekiagiza kikosi kazi kinachofanya
kazi hiyo kuhakkisha kinakamilisha uwekaji alama mifugo katika kipindi cha
mwezi mmoja.
Amewapongeza wafugaji
kujitokeza kwa wingi na hii ni kutokana na maandalizi mazuri ikiwemo Elimu ya
kutosha kabla ya zoezi kuanza.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment