Muonekano wa ndani wa gari la wagonjwa lililokabidhiwa katika kituo cha Afya Busondo Wilaya ya Nzega, mkoa wa Tabora.
Mkuu wa Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora, Mh. Geofrey Ngupula akikata utepe
kuashiria uzinduzi rasmi wa gari jipya na la kisasa la kubebea wagonjwa
lililokabidhiwa katika kituo cha Afya Busondo, Tarafa ya Puge, lililotolewa na Mbunge wa Nzega Vijijini
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na
Wazee, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla.
wakishangilia baada ya kukabidhiwa kwa gari hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora, Mh. Geofrey Ngupula akizungumza mara
baada ya kuzindua rasmi gari jipya na la kisasa la kubebea wagonjwa
lililokabidhiwa katika kituo cha Afya Busondo, Tarafa ya Puge, lililotolewa na Mbunge wa Nzega Vijijini
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na
Wazee, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla.
Mkuu wa Wilaya ya Nzega akiongozana na Naibu Waziri Kigwangalla.
Mbunge wa jimbo la Nzega
Vijijini ambaye pia ni Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amekabidhi gari maalum la kubebea
wagonjwa (Ambulance) mpya na la kisasa katika Kituo cha Afya Busondo kilichopo
Tarafa ya Puge ambalo litakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Nzega Vijijini.
Tukio hilo la kukabidhi gari
hilo limefanywa na Mkuu wa Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora, Mh. Geofrey Ngupula ambaye alitoa
agizo kali kwa Mganga Mkuu wa Kituo hicho kuhakikisha gari hilo linatumika kwa
shughuli zilizokusudiwa ikiwemo za kubebea wagonjwa na akina mama wajawazito
kuwawaisha sehemu muhimu za kutolea huduma stahiki.
Mkuu wa Wilaya huyo
alimpongeza Mbunge wa Jimbo hilo Dk. Kigwangalla kwa kuweza kuwasaidia
wananchi wa Jimbo hilo kwa kuweza
kuwasaidia gari hilo la Wagonjwa kwani
litasaidia kuokoa maisha ya wananchi hao ambao wapo maeneo ya mbali na kituo
cha Afya huku pia likitarajiwa kuwa msaada kwa kuwapeleka wateja katika ngazi za juu za huduma hiyo ikiwemo Hospitali
za Wilaya, Mkoa, Kanda na Taifa.
Aidha, alisema ni marufuku
wagonjwa kuombwa kuchangia mafuta
ya ambulance hiyo au gharama yoyote ile,
gari hili wagonjwa walitumie bure kwani limetolewa bure na pia huduma zote
zikiwemo za mafuta zinalipwa na Halmashahuri hiyo.
“Gari hilo lipatikane
kituoni wakati wote pamoja na dereva.
Tumeshahakikishiwa hapa Halmshauri imesema ina mafuta ya kutosha litakuwa
linajazwa lita 90, kila yatakapokuwa yametumika hivyo kusiwe na kisingizio
kingine cha kuweza kudai mafuta ama kuwatoza wananchi gharama na atakayefanya
hivyo Serikali hii si ya mchezo hatua kali zitafuata , tutakutumbua tu”
alieleza Mh. Ngupula.
Ameongeza kuwa gari hilo
ambalo ni la kisasa, litunzwe na kulindwa ili liweze kutumika kwa miaka mingi
ijayo na kuwa msaada kwa Tarafa hiyo na
wananchi wote watakaopata msaada.
Kwa upande wake, Dk.
Kigwangalla amewaomba wananchi waendelee kumuombea kwa kazi anayofanya ikiwemo
jukumu la kulitumikia Taifa katika nafasi yake ya Unaibu Uwaziri wa Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Dk. Kigwangalla ameishukuru
serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli kwa kuweza kuwa karibu na Wananchi ikiwemo
kushughulikia suala la maji kutoka Ziwa Victoria na kuja Mkoa wa Tabora ikiwemo
kuanzia katika Wilaya hiyo ya Nzega na kisha kwenda maeneeo mengine.
“Tunampongeza Rais wetru Dk.
Magufuli kwa kuwa karibu na wananchi wake. Tulikuwa nae Mkoani kwetu hapa
Tabora na amezindua miradi mbalimbali ikiwemo ya barabara na ule wa maji safi
yatakayotoka Ziwa Vitoria. Shida ya maji kwa wananchi wa Nzega inaenda kuwa histoa
kwani Maji hayo yatakuja hapa na kisha kwenda maeneo mengine. Rais wetu
anatupenda na tuendelee kumuunga mkono hasa juhudi zake za kulinda rasilimali
za nchi yetu na pia katika kushughulikia mafisadi na wahujumu uchumi wa Taifa
letu
Mimi Mbunge wenu pia muendelee
kuniombea na kila siku mawazo yangu na akili yangu ipo pamoja nanyi ndio maana
nimeweza kuwaletea gari hili la wagonjwa, na pia kufanikisha kuandaa kambi
maalum ya matibabu bure ya wiki moja kwa wananchi wote wa Nzega bure” alieleza
Dk. Kigwangalla.
Tukio hilo la ukabidhi wa gari
hilo pia lilishuhudiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Madiwani wa Jimbo hilo
na wale wa jimbo jirani ikiwemo Bukuene, Viongozi wa ulinzi na Usalama pamoja
na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nzega.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment