Msanii mkongwe wa muziki wa asili nchini Tanzania, Mrisho Mpoto
baada ya kufanya vizuri na wimbo ‘Sizonje’ ambao ulipendwa na watu wa
rika zote ndani ya nchi na kimataifa, hatimaye Jumatatu hii (tarehe 1
August 2017) anatarajia kuachia wimbo wake mpya ‘Kitendawili’ akiwa
amemshirikisha mkali wa nyimbo za mahaba, Kassim Mganga.
Wimbo
uliopita ‘Sizonje’ wa muimbaji huyo uliacha maswali mengi kwa wapenzi
wa muziki wake kutokana namna maishiri ya wimbo huo yalivyokuwa magumu
huku wengi wakidai huwenda wimbo huo alimuimbia Rais John Pombe Magufuli
kitu ambacho hakuwahi kukiweka wazi licha ya Rais huyo kutamka mara
kadhaa katika mikutano yake kwamba wimbo huo alikuwa kwaajili yake.
Sasa
mshairi huyo ametangaza ujio wake mpya na wimbo ‘Kitendawili’ akiwa
Kassim Mganga ikiwa ni wimbo wa kwanza ambao unawakutanisha wawili hao
ambao kila mmoja ni mkali kwa upande wake.
Mpoto
amesema amerekodi wimbo wake huo mpya katika studio za Combination
Sound chini ya producer mahiri, Man Walter ili kupata ladha tofauti ya
muziki wake.
“Mimi naamini muziki ni ladha,
nyimbo zangu nyingi nimefanya ndani ya studio yangu chini ya producer
Alan Mapigo na zilifanya vizuri. Lakini katika project hii mpya nikaona
sio mbaya kama nikibadili dhala ya beat na kupata kitu tofauti na kweli
Man Walter amefanya kitu kizuri sana, menejimenti pamoja na watu wangu
wa karibu wamefurahishwa na kile ambacho amefanya ,” alisema Mpoto.
Aliongeza,
“Pia katika wimbo huu utamsikia Kassim Mganga, huyo ni mtu mpya kabisa
katika nyimbo zangu, amefanya kitu kikubwa sana ambacho bila shaka
kitawashangaza mashabiki wengi wa muziki. Kwahiyo napenda kuwaambia
mashabiki wakae mkao wa kula, Mpoto nimerudi upya na kazi ni nzuri,”
Mjomba
amewataka mashabiki wake wa muziki kuusubiria kwa hamu wimbo huo ambao
utaachiwa siku ya Jumatatu (tarehe 1 mwezi August) kupitia mitandao ya
kijamii (blogs) pamoja na redio.
Pia mshairi
huyo amesema siku hiyo ataachia kwanza audio na baada ya siku kadhaa
atatoka video ambayo amedai ndani yake kuna mambo mengi mapya ambayo
hayajazoeleka kwenye muziki wake.
Kwa upande wa
muimbaji Kassim Mganga ambaye ameshiriki ndani project ya namna hiyo
kwa mara ya kwanza na Mrisho Mpoto, amesema amefurahishwa na namna wimbo
huo ulivyoandaliwa huku akiwataka mashabiki kusubiria muziki mzuri.
“Kusema
kweli hii ni mara yangu ya kwanza kufanya kazi ya namna hii na Mrisho
Mpoto ambaye hata mimi ni shabiki wa muziki wake. Nimefurahishwa sana na
kile tulichokifanya, binafsi nafarijika kuona ushirikiano wetu jinsi
ulivyozalisha kitu kikubwa katika muziki, natamani ngoma itoke hata
kesho ili mashabiki waone kitu ambacho nakizungumzia. Kwahiyo mashabiki
wa muziki kwa umoja wetu tusubirie muziki mzuri ambao utateka fikra na
kutoa burudani kwa mashakibiki,” alisema Kassim Mganga.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment