Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na baadhi wa Wajumbe
wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Singida, wakati alipofika katika Ofisi
ya Mkuu wa mkoa huo kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na
maofisa wa Jeshi hilo pamoja na kujua changamoto wanazokutananazo wakitekeleza
majukumu yao.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na askari na maofisa
wa Jeshi hilo na kuwataka wafanyekazi kwa kutenda haki na kusimamia misingi ya
sheria na taratibu, IGP Sirro yupo mkoani Singida kwa ziara ya kikazi yenye
lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na kujua changamoto
wanazokutananazo wakitekeleza majukumu yao.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini
(IGP) Simon Sirro, amemaliza ziara yake katika mikoa ya kanda ya ziwa pamoja na
mkoa wa Singida, huku akiacha morali kwa watendaji wa Jeshi hilo hatua ambayo
italiwezesha kufanyakazi zake kwa weledi katika kukabiliana na matishio ya
uhalifu na wahalifu.
IGP Sirro, amefanya ziara hiyo
ikiwa ni mkakati wake aliojiwekea tangu alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi hilo
kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na maofisa ili kujua namna
wanavyotekeleza majukumu yao ya kazi za Polisi.
Katika mazungumzo yake IGP
Sirro, amewataka askari na maofisa kutimiza wajibu wao kwa kutenda haki na bila
uwoga wala kumuonea mtu muhali jambo ambalo litarahisisha upatikanaji wa
taarifa za uhalifu na wahalifu katika jamii.
Hata hivyo, katika mabaraza ya
kuzungumza na askari na maofisa baadhi ya hoja kadhaa ziliibuliwa kwa baadhi ya
askari waliopata nafasi ya kutoa mawazo yao, ambapo IGP Sirro aliahidi
kuzishughulikia mapema ili kuzidisha morari katika utekelezaji wa majukumu yao
ya kila siku.
Aidha, katika ziara yake IGP
Sirro, alipata fursa ya kukutanana Wajumbe wa Kamati za Ulinzi na Usalama ya
mkoa huku masuala kadhaa ya kiusalama na mbinu na mikakati ikijadiliwa katika
kamati hizo na kuahidi kutoa ushirikiano utakaowezesha kukabiliana na matishio
mbalimbali ya kiuhalifu.