JESHI la Polisi nchini limetoa tahadhari kwa watu au vikundi vya watu vilivyopanga kufanya uhalifu klatika siku ya siku kuu ya Eid El Fitri.
Taariofa iliyotolewa na Jeshi hilo kupitia kwa Msemaji wake Advera Bulimba imewataka
wananchi kuwa makini katika suala zima la ulinzi na usalama wa maisha na mali zao.
"Kipindi kama hiki cha sikukuu baadhi ya watu
hupenda kutumia fursa hiyo kufanya vitendo vya uhalifu na vitendo vingine
ambavyo huhatarisha usalama wa watu na mali zao,"ilisema taarifa hiyo.
Naibu kamishna huyo wa Polisi, Advera Bulimba alisema Jeshi
la Polisi nchini, limejipanga kwa
kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama katika mikoa yote
kuhakikisha kwamba wananchi
wanasherehekea Sikukuu katika hali ya amani
na utulivu.
Aidha, ulinzi
umeimarishwa kwenye maeneo yote, yakiwemo maeneo ya kuabudia, fukwe za bahari,
sehemu za starehe na maeneo mengine ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya
watu.
"Vilevile, Jeshi la Polisi linawatahadharisha watumiaji
wa vyombo vya moto barabarani kuwa makini na kuzingatia sheria na kanuni za usalama
barabarani, Jeshi la Polisi halitasita
kuwachukulia hatua kwa wale wote watakaovunja
sheria na kanuni za usalama barabarani kwa mabereva kutumia vilevi,
bodaboda kubeba mishikaki, kwenda mwendo
kasi pamoja na kupiga honi hovyo," taarifa hiyo ilieleza.
Pia,
tunawataka wananchi wote kuwa wepesi
katika kutoa taarifa kwa kupitia namba za simu za bure 111 au 112 pindi wanapoona viashiria vyovyote vya
uhalifu katika maeneo yao ya makazi ama maeneo ya biashara.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment