RAIS wa pili wa Botswana
Sir Kitemure Masire amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 91.
Kufuatia msiba huo,
serikali ya Botswana imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa.
Sir
Ketumile, aliongoza taifa hilo kuanzia 1980 hadi 1998, na amekuwa akisifika kwa kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuweka
msingi imara wa uthabiti wa kisiasa katika taifa hilo.
Pia
alishiriki katika mikakati ya kufanikisha amani katika mataifa kadha Afrika,
ikiwa ni pamoja na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Msumbiji.
Botswana
ni moja ya nchi tajiri na imara zaidi barani Afrika.
Sir
Ketumile alichukua uongozi kufuatia kifo cha Rais wa kwanza wa Botswana baada
ya uhuru Sir Seretse Khama mwaka 1980.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment