MAONESHO
ya Vyuo Vikuu vya nchini India yanatarajiwa kufanyika kesho huku yakitarajiwa
kutoa fursa kwa wanafunzi wa Kitanzania kuvifahamu vyuo vilivyopo nchini humo
na ubora wa taaluma zake.
Maonesho
hayo ambayo yameandaliwa na Global Education Link (GEL) kwa kushirikiana na
Ubalozi wa India nchini yatafanyika kesho katika ubalozi huo uliopo jirani na
Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC).
Akizungumzia
maonesho hayo, Mkurugenzi wa Global Education Link, Abdulmalik Mollel amesema, wanafunzi
wa kitanzania wamekuwa wakikumbana na changamoto kubwa ya kudsoma katika vyuo
ambavyo havina ifa.
“Unakuta
mwanafunzi anapewa taarifa ambazo si sahihi hata katika vyuo anachokwenda, na
ndio sababu tumeamua kuandaa maonesho hayo ili kubaini vyuo sahihi,” alisema.
Amesema
wanafunzo wengi wamejikuta wakisoma katika vyuo ambavyo havina hadhi sawa na
ile waliyotegemea, hatua inayowawia vigumu katika kutambulika na Tume ya Vyuo
Vikuu nchini (TCU).
Kwa
upande wake Balozi wa India nchini, Sandeep Arya amesema maonesho hayo
yatafanyika Kesho na keshokutwa katika ubalozi wa India na kwamba lengo kubwa
ni kuwaunganisha wanafunzi wa kitanzania wanaolenga kusoma katika nchi hiyo na
vyuo vyenye ubora.
Arya
amesema maonesho hayo yatashirikisha taasisi 20 za vyuo vikuu ambazo zinazotoa
fani tofauti katika ngazi zote za elimu ya juu.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment