Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Harrison Mwakyembe akibonyeza kitufe
kuzindua Televisheni ya mtandaoni ya Idara ya Habari-MAELEZO jana mjini
Dodoma.Televisheni iyo itaonyesha kazi mbalimbali za Wizara,Taasisi na Idara za
Serikali.Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Anastazia Wambura.
Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Harrison Mwakyembe,Naibu Waziri wake
Anastazia Wambura,Katibu Mkuu Prof.Elisante Ole Gabriel na Mkurugenzi Mkuu
Idara ya Habari-MAELEZO Dkt.Hassan Abbas wakifurahi mara baada ya kuzindua Televisheni
ya mtandaoni ya Idara ya Habari-MAELEZO jana mjini Dodoma.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Mhe,Harrison Mwakyembe akiangalia mahojiano yaliyofanyika kati ya Mkurugenzi wa
Idara ya Maelezo Hassan Abbas na Makamu wa Rais Mhe.Samia Hassan Suluhu kuhusu
maadhimisho ya Muungano yatakayofanyika mjini Dodoma.Mahojiano hayo ni ya
kwanza kupitia televisheni ya mtandaoni ya Idara ya habari-MAELEZO.
Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe.Harrison Mwakyembe akizungumza na menejimenti ya Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo(Hawapo Pichani) na kuipongeza Idara ya habari
kwa kuwa wabunifu.Kulia kwake ni Naibu Waziri wake Anastazia Wambura,Katibu
Mkuu Prof.Elisante Ole Gabriel na Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari-MAELEZO
Dkt.Hassan Abbas
Na Daudi
Manongi-MAELEZO.
Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Harrison Mwakyembe ameipongeza Idara ya
Habari-MAELEZO kwa ubunifu mkubwa katika
kuitangaza Serikali.
Waziri
Mwakyembe ameyasema hayo jana mjini Dodoma wakati akizindua televisheni ya
mtandaoni ya Idara ya Habari-MAELEZO inayoitwa MAELEZOTV.
“Napenda nichukue
fursa hii kwa kuwapongeza Idara ya Habari kwa kazi nzuri mnayoifanya katika Wizara
hii,nawapongeza kwa ubunifu mkubwa na leo tunazindua Televisheni ya mtandaoni
ya Idara hii kwa mara ya kwanza katika
historia ya Wizara yetu na Idara ya Maelezo kwa ujumla kuwa na” Alisema Waziri
Mwakyembe.
Amesema kuwa
kwa kazi ya kwanza ambayo imeonekana katika televisheni hiyo imeonyesha weledi
wa hali ya juu na kuwataka viongozi wengine wa Wizara hiyo kuiga mfano mzuri na
kuwa wabunifu na kusisitiza kuwa nchi yetu ina vipaji na ubunifu wa hali ya juu
ikiwemo timu yetu ya Vijana ya Serengeti Boys na n.k
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO,amesema kuanzishwa kwa televisheni hii ya mtandaoni
itasaidia kwa kiasi kikubwa Serikali katika kutangaza matamko mbalimbali na
uzinduzi wake wa mapema utasaidia kufikisha taarifa mbalimbali kwa jamii
husika.
“Sisi kama
Serikali tumekuwa makini katika kuimarisha mawasiliano kati yetu na wananchi na
hii televisheni ya mtandaoni itatusaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha dhima ya
Serikali ya awamu ya tano katika kutekeleza kazi zake”,Aliongeza Dkt Abbas.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment