Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na
Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete(kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa WAMA
Bi.Zakhia Meghji wakiimba wimbo maalumu wa shule ya Sekondari ya WAMA NAKAYAMA
wakati wa mahafali ya pili ya kidato cha sita ambapo wanafunzi 45 wamehitimu.
Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu kidato cha sita katika shule ya sekondari WAMA NAKAYAMA.
Theresia Sanu (kulia)akisoma hotuba ya wahitimu kwa Mgeni Rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa mahafali ya pili ya kidato cha sita ya shule ya sekondari ya WAMA NAKAYAMA.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye mahafali ya pili ya kidato cha sita ya shule ya Sekondari ya WAMA NAKAYAMA ,ambapo aliwaasa wanafunzi hao 45 kusoma zaidi ili waje kulisaidia Taifa lao.
Mwenyekiti wa WAMA Mama Salama Kikwete akihutubia katika mahafali ya kidato cha sita ya shule ya WAMA NAKAYAMA ambapo aliwataka wanafunzi hao kusoma na kufika juu zaidi.
Wahitimu wakifuatilia hotuba mbalimbali
***************
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
amewahimiza wanafunzi kote nchini kupenda kusoma masomo ya Sayansi hasa
watoto wa kike ili Taifa liweze kujitosheleza kwa wataalamu wa fani mbalimbali
nchini hasa wakati huu ambao Taifa linaelekea kwenye uchumi wa Viwanda.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli
hiyo katika hotuba yake kwenye mahafali ya Pili ya wanafunzi wa Kidato cha Sita
wa shule ya sekondari ya WAMA- NAKANYAMA Jijini Dar es Salaam, mahafali ambayo
imehudhuriwa na wake wa Marais Wastaafu.
Makamu wa
Rais amesema haitapendeza hata kidogo ajira nyingi nchini kuchukuliwa na
wataalamu mbalimbali mataifa ya nje hasa kipindi hiki wakati Serikali inahimiza
ujenzi wa viwanda hivyo amesisitiza wanafunzi wajikite kwenye kusoma masomo ya
sayansi ili taifa liweze kujitosheleza kwa ajili ya manufaa ya maendeleo ya
taifa.
Amesema
katika kuhakikisha taifa lipata wanasayansi wengi, Serikali inaendelea na mpango
wa ujenzi wa maabara na kununua vifaa vya maabara ili kuhamasisha wanafunzi
wengi zaidi kupenda kusoma masomo ya sayansi kote nchini.
Makamu wa
Rais pia amesisitiza kuwa Serikali ya awamu ya Tano inakusudia kuimarisha
ufundishaji wa masomo ya Teknolojia ya habari na Mawasiliano –TEHAMA- katika
shule za Sekondari na kujenga maabara za kompyuta nia ikiwa ni kuongeza
wataalamu wa fani hiyo nchini.
Kuhusu
mila na desturi kandamizi kwa wanawake na wasichana zilizopo kwenye baadhi ya
jamii nchini, Makamu wa Rais ameitaka jamii kukomesha mila hizo na
iwashirikishe wanawake katika mipango na mikakati ya maendeleo ya nchi kwani
watakuwa ni chachu ya maendeleo katika jamii husika.
“Wote
tunajua wanawake ni chachu na kiungo muhimu katika maendeleo ya jamii, Taifa na
Dunia kwa ujumla hivyo ni wajibu wa jamii kushirikisha wanawake katika kupanga
na kutekeleza shughuli za maendeleo kote nchini” amesisitiza Makamu wa Rais.
Makamu wa
Rais pia ameipongeza Taasisi ya Wanawake na Maendeleo – WAMA- kwa kujenga shule
Mbili za Sekondari na kusomesha watoto wanaotoka kwenye familia maskini na
yatima na kusema huo ni mfano wa kuingwa na wadau wengine wa maendeleo katika
kusaidia kundi hilo ili watoto wanaotoka kwenye familia maskini nao waweze
kuapata elimu itakayowasaidia katika maisha yao ya baadae.
Kuhusu
changamoto zinazoikabili shule ya WAMA – NAKAYAMA, Makamu wa Rais ameahidi
kushughulikia changamoto hizo ikiwemo uhaba wa maji, ubovu wa barabara kuelekea
kwenye shule hiyo na tatizo la uhaba wa mabweni
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama
SALMA KIKWETE amesema aliamua kuanzisha taasisi hiyo ambayo inamiliki shule
Mbili mpaka sasa ili kusaidia watoto wa maskini na yatima kupata elimu bure
ambapo mpaka sasa kuna idadi kubwa ya wanafunzi wanaliohitimu katika shule hizo
ambao wamejiunga na masomo ya elimu ya juu.
Mama
Salma Kikwete ameshukuru ushirikiano mkubwa anaopata kutoka Serikalini
unaolenga kuhakikisha shule zinazoendeshwa na taaisisi hiyo ikiwemo ya Wama –
Nakayama zinafanya vizuri.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment