Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Amos Makalla akipokea taarifa ya utatuzi wa mgogoro wa ardhi baina ya wananchi wa vijiji 34 vya Hamashauri ya Mbarali na Hifadhi ya Ruaha.
Mkuu wa Mkoa akiwa na wajumbe wa Kamati
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza na wanahabari.
MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla leo amepokea taarifa ya kikosi kazi alichounda kwaajili ya kutatua mgogoro wa hifadhi ya Taifa Ruaha na Vijiji 34 vya Haashairi ya Mbarali.
Taarifa hiyo ina mapendekezo ya kurejesha mto Ruaha Mkuu katika hali ya asili kutiririsha Maji kwa ajili ya Hifadhi ya Ruaha na bwawa la Mtera.
Akizungumza wakati wa upokeaji wa taarifa hiyo, Mkuu wa Mkoa, Makalla aliwashukuru wananchi kwa kutoa ushirikiano kuanzia uwekaji wa mawe ya mipaka kwa mujibu wa GN namba 28 na ushiriki wao wa kutoa maoni.
Makalla alisema kikosi kazi alichokiunda kimefanya kazi kubwa na kwa muda muafaka wakati Makamu wa Rais ameunda kikosi kazi kingine na ameahidi taarifa hiyo itakisaidia kikosi kazi kilichoundwa.
Amewaomba wananchi kuendelea kuwa watulivu na ripoti hiyo itawasilishwa kwenye kikao cha Bodi ya ushauri cha mkoa na baadaye mapendekezo hayo yatawasilishwa kwa Rais kwa ajili ya maaumuzi.
Aidha amesema anaamini taarifa hiyo ni muhimu kwa ajili ya kumaliza migogoro ya ardhi na uhifadhi wa maeneo oevu na Hifadhi ya Ruaha.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment