Na Katuma Masamba
CHUO
Kikuu cha Dodoma (UDOM) kimetengeza mfumo wenye uwezo wa kuhakiki taarifa na
hotuba mbalimbali na kubainisha kama ni halisi au zimechezewa na wahalifu wa
kimtandao.
Hayo
yameelezwa na Mkuu wa Kitivo cha Elimu Ang’avu wa UDOM, Profesa Leonard Mselle
katika semina ya juu ya utafiti wa masuala ya usalama wa mtanadao ambapo
alisema, mtambo huo unaweza kuonesha kama taarifa ni sahihi au imechezewa.
Awali
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Dk Jim Yonazi
alisema, suala la usalama wa mtandao ni jambo muhimu hasa kwa kuzingatia
teknolojia inakua kila siku.
Alisema
kama hakutakuwa na usalama juu ya mitandao kuna hatari mbalimbali ambazo
zinaweza kujitokeza kutokana na matumizi ya mtandao.
“…Kutokana
na teknolojia ambazo zipo na nia ya serikali ya kuwekeza kwenye tafiti, leo
tumeona mbinu au mifumo mbalimbali inayotengzwa hapa nchini kwa ajili ya
kutulinda katika matumizi ya mtanadao,” alisema Dk Yonazi.
Profesa
Mselle alisema, mtambo huo una uwezo wa kuanisha taarifa kama ni halisi ambapo
ukiweka tyaarifa au hotuba unayotaka kubaini ukweli wake itaonesha kama ni
halisi au imechezewa.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment