Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda (kushoto),Balozi wa China nchini,Dk,Lu Youoing wakifunua kitambaa kuashiria uwekaji Jiwe la Msingi la ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wa Chuo cha Utalii zamani Bandari uliofanyika jana. Wengine ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam, DRFA, Almas Kasongo (wa pili kushoto), Katibu Tawala Wilaya ya Temeke,Hashim Komba (katikati) na Wa pili kulia ni Shafii Dauda. (Picha na Yusuf Badi)
**********
Na Katuma Masamba
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wachezaji wa mpira wa miguu wataanza kupimwa kama wanatumia dawa za kulevya kwa kutumia vifaa maalumu.
Wachezaji hao ni wanaoshiriki katika mashindano ya Ndondo Cup, yanayofanyika jiji Dar es Salaam huku akiweka wazi watakaobainika kutumia dawa za kulevya watazuiwa kuingia uwanjanj na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Makonda ametoa kauli hiyo leo wakati Balozi wa China nchini, Dk Lu Youqing akiweka jiwe la msingi katika uwanja wa Chuo cha Taifa cha Utalii kuashiria ujenzi wa uwanja huo.
Vifaa hivyo vitatumika kupima matumizi ya dawa za kulevya aina ya Bangi, Heroin na Cocaine pamoja na dwa zingine.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment