Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Wednesday, 28 February 2018

RC MWANRI APOKEA VIFAA VYA UTUNZAJI MAZINGIRA

 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akizungumza mara baada ya kupokea vifaa mbalimbali vya thamani ya milioni 4.4 ambavyo vitasaidia katika kampeni ya uhifadhi mazingira na upandaji miti . Vifaa hivyo vimekabidhiwa jana na  Kampuni ya Alliance One Tobacco Tanzania Ltd.


Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(mwenye koti  la bluu)  akipokea  vifaa mbalimbali vyenye thamani ya milioni 4.4 ambavyo vitasaidia katika kampeni ya uhifadhi mazingira na upandaji miti . Vifaa hivyo vimekabidhiwa jana na  Kampuni ya Alliance One Tobacco Tanzania Ltd.



Baadhi ya vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 4.4 vilivyotolewa jana na  Kampuni ya Alliance One Tobacco Tanzania Ltd kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Mkoa wa Tabora za kampeni yake ya kuhakikisha eneo hilo linakuwa la kijani kwa kupanda miti kwa wingi. Picha na Tiganya Vincent


WAZIRI MKUU AZINDUA BARABARA YA TANDAHIMBA MJINI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la barabara ya Tandahimba mjini, Mkoani Mtwara, yenye urefu wa kilomita tatu, ilityojengwa kwa fedha za halmashauri, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wananchi wa Wilaya ya Tandahimba, wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozungumza nao, mara baada ya kuweka jiwe la msingi la barabara ya Tandahimba mjini, Mkoani Mtwara, yenye urefu wa kilomita tatu, ilityojengwa kwa fedha za halmashauri, Februari 28, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi, mara baada ya kuweka jiwe la msingi la barabara ya Tandahimba mjini, Mkoani Mtwara, yenye urefu wa kilomita tatu, ilityojengwa kwa fedha za halmashauri, Februari 28, 2018.


CCM MANISPAA YA IRINGA YATEKELEZA AHADI YA MBUNGE MSIGWA KATIKA SOKO KUU LA MANISPAA YA IRINGA.

Mwenyekiti wa chama cha mapindizi (CCM) manispaa ya Iringa Said Rubeya akimkabidhi TV na king'amuzi mwenyekiti wa masoko ya manispaa ya iringa Starmi Mathew akiwa sambamba na viongozi na wanachama wa chama hicho
Mwenyekiti wa chama cha mapindizi (CCM) manispaa ya Iringa Said Rubeya akimkabidhi king'amuzi mwenyekiti wa masoko ya manispaa ya iringa Starmi Mathew akiwa sambamba na viongozi na wanachama wa chama hicho
Mbunge wa viti maalumu ritta Kabati akiwa na diwani wa kata ya Mshindo Ngwada pamoja na matha walipokuwa wakikabidhi TV na king'amuzi cha Azam kwa viongozi wa soko kuu la manispaa ya Iringa
Wananchama wa chama cha mapinduzi pamoja na baadhi ya wafanyabiashara walipohudhuria hafla ya kukabidhiwa kwa TV na king'amuzi cha Azam TV kwa viongozi wa soko kuu manispaa ya Iringa.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

CHAMA cha mapindizi (CCM) manispaa ya Iringa kimetekeleza ahadi ilikuwa imeahidiwa na chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wakati wa kampeni za mwaka 2015 ya kuwatafutia TV wafanyabiashara wa soko kuu la manispaa ya Iringa chini ya mgombea wake wa ubunge mchungaji Petter Msigwa ambaye kwa sasa ndio mbunge wa jimbo la Iringa mjini 
 
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa CCM manispaa ya Iringa Said Rubeya alipokuwa anakabidhi TV nchi 58 na king’amuzi kwa kiongozi wa masoko hapa manispaa.

Rubeya alisema kuwa wametoa TV hiyo kwa lengo la kuhakikisha kuwa wananchi na wafanyabiashara wa soko hilo wanapata habari kwa wakati.

“Mimi nimekuja jana hapa mkaniambia kero hii nikaichuklua na chama change kimeifanyia kazi haraka iwezekanavyo na saizi tumekuja kukabidhi” alisema Rubeya

Rubeya alisema kuwa chama cha mapinduzi kinaamini kwenye utendaji na sio kulalamika na kuandamana hivyo kuna tumia vizuri falsafa ya Rais Dr John Pombe Magufuli ya hapa kazi tu ndio maana tupo hapa kufanya kazi kwa vitendo kwa wananchi.

“Chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa kinafanya kazi kwa vitendo pale tunaposikia kero za wananchi tunatafuta njia za kutatua changamoto hizo ndio maana leo tunaleta hii TV na king’amuzi ili wafanyabiasha mpate habari mkiwa hapa kazini” alisema Rubeya

Rubeya alisema kuwa alipokea malalamiko kutoka kwa wafanyabiasha ya kutekelezwa kwa ahadi ambazo zilizotelewa na mbunge wakati kampeni na imepita miaka mingi haijatekelezwa hivyo wakaamua kuichua na kuitatua ili kuwapa haki wananchi na wafanyabishara wa soko hilo.

“CCM tukitoa ahadi tunatekeleza kwa wakati lakini wenzetu wamekuwa wanapiga propaganda tu za maneno hivyo wananchi mnatakiwa kuchagua viongozi ambao wanaweza kutekeleza ahadi zao kwa maendeleo ya wananchi wanaowangoza” alisema Rubeya

Kwa upande wake mbunge wa viti maalumu ritta Kabati alisema kuwa kitendo cha leo walichokifanya chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa kinaonesha kuwa chama hicho ni chama cha wananchi wote ndio maana leo wametoa TV na king’amuzi kwa ajili ya kupata habari kwa wananchi wanaopata huduma katika soko hilo.

“Kupata habari ni haki ya kila mwananchi wa mtanzania anapata habari kwa wakati hivyo kutoa TV hii kutasaidia kuongeza wigo kwa wananchi kupata habari kwa wakati” alisema Kabati

Kabati aliwataka viongozi wa soko hili kuandaa mkutano wa kusikiza kero ili kuzitafutia ufumbuzi kwa lengo la kuendelea kukuza uchumi na kuleta maendeleo kwa haraka zaidi na kuendana na kasi ya Rais wa awamu ya tano Dr Johh Pombe Magufuli.

“Mwenyekiti naomba mniandalie mkutano nije kuwasikiliza kero zenu kwa kuwa ni haki yenu na msipofanya hivyo mtakuwa mnajinyima haki yenu ya msingi ya kutatuliwa kero zenu” alisema Kabati

Naye mwenyekiti wa masoko ya manispaa ya iringa Starmi Mathew aliwashukuru chama cha mapinduzi kwa msaada walioutoa kwa kuwa wamerahisisha wafanyabiashara kupata habari wakiwa kazini.

Mathew alikiomba chama hicho kuongezea nguvu kwenye masoko mwengine ya manipsaa ya Iringa kupata hata TV ndogo hata kama sio kuwa kama ambayo imetolewa leo katika soko kuu la manispaa ya Iringa

“Naomba nimbe kama hapo mbe mtapa nguvu nyingine basi tunaomba mtukumbuke tena maana kuna soko hilo hapo chini nalo linahitaji kuwa na Tv nao wewe kupata habari kama haki yao ya msingi kujia nini kinaendelea duniani” alisema Mathew

Aidha Mathew akawamba viongozi wa CCM kuwasidia kuiomba SUMATRA kutengeneza njia ya daladala ipite katika soko hilo ili kuongeza mzunguko wa kibiashara kama ilivyo mikoa mingi hapa nchini.


WATAALAM WA AFYA MOJA KUANDAA MPANGO MKAKATI WA ULINZI NA USALAMA WA VIMELEA HATARISHI


Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiru Taratibu akieleza jambo wakati wa Mkutano wa wataalamu wanaounda Mtandao wa Huduma za Maabara nchini, uliojikita katika ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi leo Februari 28, 2018 mjini Morogoro.

Mtaalamu Masuala ya Mpango Mkakati wa Maabara kutoka Shirika la Maabara –SANDIA, Laura Jones, akifafanua umuhimu wa Mpango huo wakati wa Mkutano wa wataalamu wanaounda Mtandao wa Huduma za Maabara nchini, uliojikita katika ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi leo Februari 28, 2018 mjini Morogoro.

Baadhi ya Wataalamu wanaounda Mtandao wa Huduma za Maabara nchini, wakijadiliana namna ya kuandaa Mpango Mkakati wa ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi, leo Februari 28, 2018 mjini Morogoro.

Wataalamu wa Afya moja wanaounda Mtandao wa Huduma za Maabara nchini wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano wa kuandaa Mpango Mkakati wa ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi, leo Februari 28, 2018 mjini Morogoro.
 ********************
Na. Mwandishi Maalum.
Wataalam wa Afya moja nchini ambao ni wataalam wa sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wameanza kuandaa Mpango Mkakati wa ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi utakaosaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa sampuli za vimelea hivyo hatarishi kutoweza kueeneza magonjwa kwa binadamu.

Mpango huo utatoa mwongozo wa namna sekta za Afya nchini ambazo ni sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira kushirikiana katika kuvichukua vimelea kwa wanyama, binadamu na mimea au wakati wa kuvisafirisha na kuvipeleka maabara kwa ajili ya Uchunguzi na wakati wa kuviharibu mara baada ya kuvifanyia uchunguzi.

Akiongea wakati wa Mkutano wa wataalamu wanaounda Mtandao wa Huduma za Maabara nchini, leo Februari 13,2018 mjini Morogoro, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiru Taratibu alibainisha kuwa serikali imedhamiria kuijenga jamii yenye Afya bora kwa kuikinga na majanga yatokanayo na magonjwa ya mlipuko hivyo imeamua kuandaa mpango huo ili kuboresha uratibu.

Naye mratibu wa Mkutano huo anayeshughulikia masuala ya Ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi katika wizara ya Afya, Jacob Lusekelo, alibainisha mpango huo ambao utatoa mwongozo wa sekta za Afya kushirikiana utasaidia kupunguza maabukizi ya vimelea hivyo kwa wanyama na binadamu.

Februari 13, 2018, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alizindua Dawati la Uratibu la Afya moja chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, likiwa na lengo la kusimamia na kuratibu shughui za Afya moja nchini, ikiwemo wataalamu wanaounda Mtandao wa Huduma za Maabara nchini, ambao unawajumuisha wataalamu wa kutoka katika sekta zote za afya katika masuala ya maabara.

Afya Moja ni dhana inayojumuisha sekta ya afya ya binadamu , wanyamapori, mifugo na mazingira katika kujiandaa , kufuatilia na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu ,wanyamapori na mifugo. Kwa kutambua umuhimu huo Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Dawati la Uratibu wa Afya moja kwa kushirikiana na Shirika la Maabra SANDIA na DTRA wameandaa mkutano wataalam hao.


Tuesday, 27 February 2018

JAFO ATOA SIKU SABA HALMASHAURI ZIKAMILISHE MIPANGO KAZI YAO



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Sulemani Jafo ametoa siku saba kwa halmashauri zote nchini kukamilisha mipango ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyo michache itakayotekelezwa kwa asilimia 100.

Akizungumza leo mjini Dodoma wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha kujadili mpango wa utekelezaji wa Miradi ya Fedha za Maendeleo za Serikali za Mitaa(LGDG) iliyoboreshwa kwa mwaka wa fedha 2017/2018 na kushirikisha wakurugenzi, wenyeviti wa Halmashauri, maafisa mipango na makatibu tawala wasaidizi wa afya.



Alisema serikali inatarajia kutoa Sh bilioni 251 za maendeleo kwa ajili ya serikali za kipaumbele cha kwanza kikiwa ni afya iliyotengewa Sh bililioni 69.

Katibu Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mussa Iyombe akizungumza na kuwataka maafisa mipango kufanya kazi yao kwa kuzingatia taaluma na kuacha kuwa na nidhamu ya woga katika kuweka mipango katika halmashauri zao. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.


WASHIRIKA WA MAENDELEO WAAHIDI KUSHIRIKIANA KWA KARIBU ZAIDI NA TANZANIA KULETA MAENDELEO


Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango,Doto James (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Shirika la Misaada ya Maendeleo la Marekani- USAID, Andy Karas, Mjini Dodoma, walipokutana kujadili namna Serikali na Washirika wa Maendeleo wanavyoweza kuimarisha ushirikiano wa kimkakati zaidi ili kuiwezesha nchi kuharakisha maendeleo yake kwa manufaa ya wananchi wake.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango,Doto James (kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi na Somalia, Bella Bird, Mjini Dodoma, walipokutana kujadili namna pande hizo mbili zinavyoweza kuimarisha ushirikiano wa kimkakati zaidi ili kuharakisha maendeleo ya nchi.

Meza Kuu ikiongozwa na Mwenyekiti wa Mkutano kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James (wa tatu kulia), kushoto kwake ni Mwenyekiti Mwenza na Mratibu wa Umoja wa Mataifa na kiongozi wa washirika hao wa Maendeleo,Alvaro Rodriguez, mjini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi,Doroth Mwanyika (kulia) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (Sera) Dkt. Khatibu Kazungu, wakifuatilia kwa makini mkutano kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo uliofanyika  Mjini Dodoma. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.


NAIBU WAZIRI MAVUNDE AAGIZA WAKURUGENZI KUPANDISHWA KIZIMBANI JIJINI MWANZA, NI KWA KUTOJISAJILI NA WCF



NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mwanza

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony Mavunde, (pichani juu), ameagiza waajiri ambao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kufanya hivyo, vinginevyo wafikishwe mahakamani mara moja.

 Mhe. Mavunde ametoa agizo hilo Jumatatu Februari 26, 2018 baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jijini Mwanza, kubaini waajiri ambao bado hawajatekeelza takwa la kisheria kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia Kwa Wafanyakazi, Sura 263 marejeo ya mwaka 2015, ambayo inamtaka kila mwajiri kutoka sekta ya umma na binafsi Tanzania bara awe amejisajili na kuwasilisha michango kwenye Mfuko huo.



Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo, Bw. Anslem Peter,  jiji la Mwanza pekee lina waajiri 1228, lakini kati ya hao ni waajiri 482 tu ndio waliojisajili na Mfuko huku waajiri wengine 746 wakiwa bado hawajajisajili. Hali hiyo ndiyo iliyomfanya Mhe. Naibu Waziri kufanya ziara hiyo ya ghafla. BOFYA HAPA KUONA ZAIDI.


Friday, 23 February 2018

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI MBALIMBALI NCHINI UGANDA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kupiga picha ya pamoja na Mawaziri pande zote mbili za Kenya na Tanzania mara baada ya kikao chao Kampala nchini Uganda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir kabla ya mazungumzo yao jijini Kampala.
 Rais Dk John Magufuli mazungumzo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Tanzania, Benjamin William Mkapa ambaye ni mratibu wa mazungumzo ya amani ya mgogoro wa Burundi
Rais Dkt. John Magufuli na Rais wa Uhuru Kenyatta wamewaagiza Mawaziri wa Tanzania na Kenya kutatua tofauti ndogondogo zinazojitokeza katika biashara kati ya nchi hizi mbili. 

Marais hao wametoa maagizo hayo leo asubuhi tarehe 23 Februari, 2018 walipokutana na kufanya mazungumzo katika hoteli ya Munyonyo mjini Kampala muda mfupi kabla ya kuanza kwa vikao vya mkutano wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Rais Magufuli na Rais Kenyatta wamesema wanataka kuona biashara kati ya Tanzania na Kenya inazidi kukua na bidhaa zinauzwa na kununuliwa baina ya nchi hizo bila vikwazo vyovyote na hivyo kuagiza tofauti zilizojitokeza katika baadhi ya bidhaa zimalizwe. 

“Kuna mambo madogomadogo yanakuwa yanajitokeza katika biashara kati ya Kenya na Tanzania, tunataka kwa haya yote Mawaziri wa Kenya na Mawaziri wa Tanzania mkae myatatue, sisi hatuna tatizo, mambo mengine madogomadogo mno, mambo ya viatu, nguo, ngano, gesi ni madogo sana, mnatakiwa myatatue nyinyi yasifike kwetu, sisi huku tuko sawasawa” amesema Mhe. Rais Magufuli na kuungwa mkono na Mhe. Rais Kenyatta.

Wametoa maagizo hayo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Monica Juma na Waziri wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Ushoroba wa Kaskazini wa Kenya, Peter Munya. 

Wakati huo huo, Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Sudani Kusini,  Salva Kiir Mayardit katika hoteli ya Munyonyo Mjini Kampala. 

Baada ya Mazungumzo hayo,  Rais Magufuli amesema Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingine za Afrika Mashariki inaguswa na hali ya Sudani kusini na ametoa wito kwa pande zinazopingana kumaliza tofauti zao ili wananchi wa Sudani Kusini wajikite kujenga nchi yao. 

“Nimemhakikishia Rais Salva Kiir kuwa Tanzania ipo pamoja na Sudani Kusini na tunapenda tofauti zinazosababisha matatizo nchini mwake ziishe, sisi Tanzania tupo tayari kufanya biashara na Sudani Kusini, hata chakula kama wanahitaji tutawauzia” amesema, Rais Magufuli. 

Kwa upande wake, Rais Salva Kiir Mayardit amesema Tanzania na Sudani Kusini zina uhusiano wa kihistoria tangu enzi ya Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na kwamba japo kuna vita nchini mwake,  Rais Magufuli amemhakikishia kuwa uhusiano na ushirikiano huo utaendelezwa na kukuzwa zaidi. 

Katika hatua nyingine,  Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Burundi Gaston Sindimwo.  

Gaston Sindimwo amemfikishia ujumbe wa Rais wa Burundi  Pierre Nkurunziza kuwa hali ya Burundi ni shwari na Mhe. Rais Magufuli amesema anafurahi kuona sasa wakimbizi wa Burundi waliokuwa wamepata hifadhi Tanzania wameanza kurudi nchi kwao.

Rais Magufuli pia amefanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Tanzania, Benjamin William Mkapa ambaye ni mratibu wa mazungumzo ya amani ya mgogoro wa Burundi aliyealikwa kuhudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hapa Kampala.


HAKUNA KUCHUKUA MAENEO BILA KULIPA FIDIA –NAIBU WAZIRI ANGELINA MABULA


Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina mabula akiwa katika ziara yake mkoani Mara.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina mabula akizungumza na watumishi wa halmashauri za Mji na Wilaya ya musoma mkoa wa Mara.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina mabula akikagua mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi katika halmashauri ya manispaa ya Musoma mkoa wa Mara.
Baadhi ya watumishi wa halmashauri ya manispaa ya Musoma wakimsikiliza Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina mabula wakati wa ziara yake mkoa wa Mara. (Picha na WANMM)
**************
Na Mwamdishi Maalum – Musoma
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Mkazi Angelina Mabula amesema ni marufuku halmashauri kuchukua maeneo ya wananchi bila ya kuwalipa fidia.
 
Mabula amesema hayo Wilayani Butiama mkoa Mara wakati wa ziara yake yenye nia ya kutatua migogoro ya ardhi pamoja na kukagua mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi.

Amesema wakati wa mchakato wa kuchukua maeneo ya mwananchi ni vyema wahusika wakashirikishwa kuanzia hatua ya awali sambambana na kuelimishwa juu ya zoezi hilo ili kuepuka migogoro inayoweza kutokea.

‘’cha msingi ni kuanza kuzungumza na mwananchi kabla ya kuchukua eneo lake na kumueleza eneo ambalo ataachiwa na halmashauri zihakikishe mwananchi huyo anapimiwa pamoja na kupatiwa hati yake’’ alisema Mabula

Aidha,  Mabula amesema eneo litakalochukuliwa na halmashauri viwanja vyake kuuzwa fedha itakayopatikana halmashauri ihakikishe inatumika katika kutengeneza miundo mbinu na huduma nyingine za jamii na kusisitiza kuwa kwa kufanya hivyo migogoro haiwezi kutokea.

Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ameziagiza halmashauri kuhakikisha zinapanga miji kulingana na ‘master plan’ ili kuwa miji bora iliyopangika